Sera za Uwekezaji Vitega Uchumi

中国国际广播电台


  

 

China ni moja kati ya nchi zinazovutia vitega uchumi vingi duniani. Katika hali ambayo uchumi wa dunia umezorota na uwekezaji wa kimataifa unapungua kwa kiwango kikubwa, China imeweza kupata mafanikio makubwa katika kuvutia mitaji ya nchi za nje. Sababu kubwa ya mafanikio hayo inatokana na kuwekwa sera nyingi mwafaka za uwekezaji.

Tangu mwanzoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, China imetenga nguvukazi, vifaa na fedha nyingi katika ujenzi wa miradi mingi ya miundo-mbinu ili kuanzisha mazingira bora ya uwekezaji na kujenga viwanda kwa wafanyabiashara wa nchi za nje. Katika muda huo, China ilitoa sheria na kanuni zaidi ya 500 za kiuchumi zinazowahusu wafanyabiashara wa nchi za nje ambazo zimeweka wajibu na dhamana ya sheria kwa uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni hapa nchini. Mwishoni mwa mwaka 1997, China ilirekebisha “Orodha ya maelekezo ya uwekezaji kwa wafanyabiashara wa kigeni” ili kuwapa motisha na kuwaunga mkono wawekeze katika maeneo ya ustawishaji wa mambo ya kilimo, nishati, mawasiliano, vifaa na malighafi muhimu, teknolojia mpya za kiwango cha juu, matumizi ya rasilimali na hifadhi ya mazingira. Kutokana na kanuni za Shirika la Biashara Duniani WTO na ahadi ilizotoa China kwa nchi za nje, nyaraka za kisheria kiasi cha 2,300 zilichambuliwa na kurekebishwa, ambazo 830 kati yake zilitenguliwa, 325 zilirekebishwa, ambapo kwa hatua ya mwanzo, kazi za kuchambua na kurekebisha sheria na kanuni za kiuchumi zinazowahusu wafanyabiashara wa kigeni zilikamilika, na utaratibu wa sheria kuhusu uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni, ambazo sheria tatu muhimu kuhusu viwanda vya ubia na vya ushirikiano kati ya China na wafanyabiashara wa kigeni pamoja na vya mitaji ya wafanyabiashara wa kigeni kuwa ni uti wa mgongo, umejengwa kwa ujumla. Hadi mwishoni mwa mwaka 2003, wafanyabiashara wa kigeni kutoka nchi na sehemu zaidi ya 170 duniani wamewekeza hapa nchini, hivi sasa idadi ya viwanda vilivyowekezwa na wafanyabiashara wa kigeni ni zaidi ya laki 4; makampuni na mashirika makubwa ya kimataifa yanavutiwa na soko la China, mashirika makubwa ya kimataifa yanayochukua nafasi 500 za juu duniani, karibu yote yamewekeza nchini China. China imechukuliwa na wawekezaji na sekta za mambo ya fedha kuwa moja ya nchi yenye mazingira bora sana ya uwekezaji.