Maeneo ya kuweka bidhaa zinazosafirishwa
nchi za nje, yaliidhinishwa
na baraza la serikali la kuendeleza
biashara ya kimatafa na shughuli
kuhusu bidhaa zinazosafirishwa
nchi za nje, ambayo yanafanana
na maeneo ya biashara huria
duniani, katika maeneo hayo,
wafanya biashara wa kigeni wanaruhusiwa
kuendesha biashara za kimataifa,
kujenga mabohari ya kuwekea
bidhaa zinazosafirishwa nje,
na shughuli za ushindikaji na
usafirishaji. Hivi sasa nchini
China kuna maeneo 15 ya bidhaa
za kusafirishwa nje, likiwemo
lile la Waigaoqiao la Shanghai.
Maeneo hayo yamekuwa kama kiunganishi
kipya kati ya uchumi wa China
na dunia.