Kutumia Mitaji ya Nje 

中国国际广播电台


       
China inatumia mitaji ya nchi za nje kwa njia za aina mbalimbali, ambazo kwa jumla zinaweza kugawanyika katika mafungu matatu. Fungu la kwanza ni kupata mikopo ya nchi za nje, ikiwa ni pamoja na kukopeshwa na serikali za nchi za nje, mashirika ya fedha duniani, benki za biashara za nchi za nje na kutoa hati zenye thamani za dhamana ya serikali kwa nchi za nje. Fungu la pili, kuwekezwa moja kwa moja na wafanyabiashara wa kigeni, vikiwemo viwanda vya ubia, vya ushirikiano na vya wafanyabiashara wa kigeni; Fungu la tatu ni uwekezaji wa aina nyingine wa wafanyabiashara wa kigeni, ambao ni pamoja na ukodishaji, biashara yenye ruzuku, kazi za usindikaji na uuzaji wa hisa.
Kutoka mwaka 1990 hadi mwaka 2001, China ilitumia mitaji ya nchi za nje dola za kimarekani bilioni 510.8, ambayo ile iliyowekezwa moja kwa moja na wafanyabiashara wa kigeni ilikuwa dola za kimarekani bilioni 378. Mitaji ya kigeni iliyotumiwa na China mwaka 2002, ilikuwa dola za kimarekani bilioni 55, ambayo ile iliyowekezwa moja kwa moja na wafanyabiashara wa kigeni ilikuwa dola za kimarekani 52.7, China ilichukua nafasi ya kwanza katika kutumia mitaji ya nchi za nje. Mwaka 2003, uwekezaji wa wafanyabiashara wa kigeni nchini China ulidumisha ongezeko kubwa, ambapo kampuni 41,081 za wafanyabiashara wa kigeni ziliidhinishwa kuanzishwa nchini China, kiasi hiki kilikuwa ni ongezeko la 20.2% kuliko mwaka uliopita; Thamani ya mikataba ya biashara iliyosainiwa ilikuwa dola za kimarekani bilioni 115.1, ambazo ni ongezeko la 39.0%; Mitaji iliyotukika hasa ilikuwa dola za kimarekani bilioni 53.5, ikiwa ni ongezeko la 1.4%.