Bima na Usimamizi Wake

中国国际广播电台


     
Shughuli za bima baada ya kuzorota kwa miaka 29, zilianza kurejea katika hali ya zamani toka mwaka 1980. Mwaka 1981, Shirika la Bima la China, ambalo hapo zamani ilikuwa idara moja ya serikali, lilianzisha matawi yake kutoka mikoa na miji inayodhibitiwa moja kwa moja na serikali kuu hadi wilaya. Kampuni za bima zinazojulikana kwa Usalama na Pasifiki, ambazo shughuli zake hasa ziko katika sehemu ya pwani ya China, zilianzishwa mwaka 1988. Mwaka 1996, Shirika la Bima la China lilipiga hatua moja kubwa katika kubadilisha utaratibu wa usimamizi na uendeshaji wa kazi, na kuungana na masoko ya kimataifa. Kuanziashwa kwa “Sheria ya bima” mwaka 1985 na kuanzishwa kwa kamati ya usimamizi wa shughuli za bima ya China mwaka 1988, kumeweka mujibu wa sheria na kanuni za uendeshaji kazi kwa shughuli za bima nchini.
Hivi sasa, hapa nchini kuna kampuni za bima na wakala wa bima zaidi ya elfu 70, ambazo zimeanzishwa bima za uzeeni, afya, ajali na mali. Hivi sasa kuna kampuni za bima za kigeni zaidi ya 30 nchini China, wakati kampuni zaidi ya 100 za nchi za nje zimefungua ofisi zake nchini, zikitarajia kuingia katika soko la bima ya China. Katika mwaka 2003, pato la kampuni za bima za nchi za nje nchini China lilikuwa Yuan zaidi ya bilioni 388, likiwa ni ongezeko la 27.1%.