Mradi wa Magenge Matatu 

中国国际广播电台


     
Mto Changjiang una rasimali kubwa ya maji, mradi wa maji wa Magenge Matatu ni mradi muhimu wa kupunguza tatizo la maji na kustawisha mto Changjiang. Mradi wa Magenge Matatu uko katika sehemu ya Sandouping, ya mji wa Yichang, mkoa wa Hubei, sehemu ya kati ya mto Changjiang. Katika sehemu hiyo Mto Changjiang ni mpana, chini yake kuna mawe magumu na makubwa ya granite, yanayoweza kudhibiti maji ya sehemu ya juu ya mto yenye eneo la kilomita za mraba 100, ambapo maji yanayopita huko ni mita za ujazo karibu bilioni 500 kwa mwaka.


Ujenzi wa mradi wa maji wa Magenge Matatu unatumia mpango wa kukamilishwa moja kwa moja, kulimbikiza maji kwa viplindi mbalimbali, na kuhamisha wakazi hatua kwa hatua. Sehemu ya juu ya ukingo wa maji ya bwawa ina urefu wa mita 3,035, maji baada ya kulimbikizwa katika hali ya kawaida ni yanakuwa na kina cha mita 175. Bwawa la maji la mradi huo linaweza kulimbikiza jumla ya mita za ujazo bilioni 39.3.

Baada ya ujenzi wake kukamilika, mradi wa Magenge Matatu utakuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia mafuriko, kuzalisha umeme, kuendeleza uchukuzi, ufugaji samaki, utalii, kuhifadhi mazingira ya asili, kuboresha mazingira, kuhamisha wakazi katika maeneo ya ustawishaji, kupeleka maji kutoka sehemu ya kusini kwenda sehemu ya kaskazini na kumwagilia maji mashamba.