中国国际广播电台
Sehemu ya kusini ya China Ina
maji mengi, lakini sehemu ya
kaskazini ina upungufu wa maji.
Ili kupeleka maji ya sehemu
ya kusinii kwa sehemu ya kaskazini
yenye ukame, wanasayansi na
wahandisi wa China walifanya
uchunguzi na upimaji porini
kwa miaka 50.
Maji ya sehemu ya kusini
yanapelekwa sehemu ya kaskazini
kwa njia tatu za mashariki,
kati na magharibi, ambazo
zinakutana na mito minne mikubwa
ya Changjiang, Manjano, Huai
na Hai, ili kugawa rasilimali
ya maji kufuatana na hali
halisi.
Njia ya mashariki: kuchukua
maji ya mto Changjiang katika
mji wa Yangzhou, ulioko sehemu
ya chini ya mto Changjiang,
kupelekwa sehemu ya kaskazini
kwa kupitia mfereji kati ya
Beijing na Hangzhou na mito
mingine inayokwenda sambamba
nao, na kuungana na maziwa
ya Hongze, Luoma, Nansi na
Dongping. Maji yanayoletwa
kutoka sehemu ya kusini yatapelekwa
kwa njia mbili ndogo, ambazo
moja ni inaelekea sehemu ya
kaskazini kupitia mto Manjano;
na njia nyingine inaelekea
upande wa mashariki hadi Yantai
na Weihai, mkoani Shandong.
Njia ya katikati inachukua
maji kutoka bwawa la maji
la Danjiangkou, kuelekea sehemu
ya kaskazini sambamba na njia
ya reli kati ya Beijing na
Guangzhou hadi miji ya Beijing
na Tianjin.
Njia ya magharibi ni kuchukua
maji kutoka bwawa la maji
litakalojengwa karibu na mto
Tongtian, tawi la mto Yalong
na mto Dadu katika sehemu
ya juu ya mto Changjiang,
na kuyapeleka hadi sehemu
ya juu ya mto Manjano. Uwezo
wa kupeleka maji kwa njia
hizo tatu ni mita za ujazo
bilioni 44.8 katika mwaka
2050, ambazo njia ya mashariki
ni mita za ujazo bilioni 14.8,
njia ya kati ni bilioni 13
na ya magharibi ni mita za
ujazo bilioni 17.
Ujenzi wa mradi huo wa kupeleka
maji unafanywa kwa vipindi
tofauti kufuatana na hali
halisi. Hivi sasa ujenzi umeanza
katika sehemu nne za njia
za mashariki na kati.
|