中国国际广播电台
Gesi ya sehemu ya magharibi
inayotoka katika mikoa ya Xinjiang,
Qinghai, Sichuan na ukanda wa
Eerduosi, inatarajiwa kupelekwa
sehemu ya mashariki ya delta
ya mto Changjiang.
Sehemu za kati na magharibi
za China kuna mabonde 6 yenye
mafuta ya asili ya petroli
na gesi, ambayo ni pamoja
na Talimu, Zhengeer, Duha,
Chaidamu, Eerduosi na Sichuan.
Rasilimali za gesi zinakadiriwa
kuwa ni mita za ujazo bilioni
2.24 na kuchukua 58.9% ya
jumla ya rasilimali za gesi
ya China, ambayo ni mita za
ujazo trilioni 3.8. Kutokana
na hali ya rasilimali za gesi,
pamoja na uchunguzi na upimaji
wa hivi sasa, serikali imeamua
kuanzisha ujenzi wa mradi
wa kupeleka gesi ya sehemu
ya magharibi kwenye sehemu
ya mashariki, kuharakisha
ujenzi wa kutandika mabomba
ya kupelekea gesi, licha ya
kujenga njia ya mabomba ya
kupelekea gesi kutoka mkoa
wa Shanxi katika sehemu ya
Beijing, zitajengwa njia 3
za kupelekea gesi ya asili
kutoka Talimu kwenda Shanghai,
kutoka Sebei ya mkoa wa Qinghai
kwenda Xining na Lanzhou,
na kutoka wilaya ya Zhong
ya Chongqing kwenda mji wa
Wuhan mkoani Hubei, ili kubadilisha
hali bora ya rasilimali kuwa
hali bora ya uchumi na kukidhi
mahitaji ya haraka ya sehemu
ya mashariki kwa gesi ya asili.
Aidha, kutokana na mpango
unaobuniwa hivi sasa, mabomba
ya kupelekea ges kutoka Seberia
ya magharibi ya Russia, yataungana
na mabomba makubwa ya kupeleka
gesi ya mradi wa kupeleka
gesi ya sehemu ya magharibi
kwa sehemu ya mashariki. Mbali
na hayo, mpango mwingine unabuniwa
hivi sasa wa kuchukua gesi
ya Seberia ya mashariki ya
Russia, nchi hizo pia zinahesabiwa
kama ni kupeleka gesi ya sehemu
ya magharibi katika sehemu
ya mashariki.
Kwa namna nyingine, kupeleka
gesi ya sehemu ya magharibi
katika sehemu ya mashariki
ni mradi wa kupeleka gesi
kutoka sehemu ya Talimu ya
mkoa wa Xinjiang katika delta
ya mto Changjiang ya Shanghai.
Njia hiyo ya mabomba, ambayo
ina urefu wa kilomita 4,200,
na mabomba yenye mpenyo milimita
1118, inapitia mikoa 8 ikiwemo
Xinjiang, Jiangsu na mji wa
Shanghai, uwezo wake wa kupeleka
gesi ni mita za ujazo bilioni
12, na kugharimiwa Yuan bilioni
120.
Hivi sasa, ujenzi wa mradi
wa kupeleka gesi umekamilishwa
kwa 48%, na ujenzi wa sehemu
ya mashariki ya njia ya mabomba
umekamilika kabisa, na kuanza
kupeleka gesi ya asili sehemu
ya mashariki ya China.
|