中国国际广播电台
Mradi wa kupeleka umeme kutoka
sehemu ya magharibi kwenda sehemu
ya mashariki ni mradi kwa ajili
ya kupeleka umeme mwingi kutoka
sehemu ya magharibi kwenda sehemu
iliyoendelea ya mashariki. Kwa
kuwa sehemu nyingi za uzalishaji
wa umeme ziko katika sehemu
za magharibi na kaskazini, lakini
matumizi ya nishati ya umeme
yako katika sehemu zilizoendelea
za kandokando ya reli kati ya
Beijing na Guangzhou na upande
wa mashariki ya njia hiyo ya
reli.
Mradi wa kupeleka umeme wa
magharibi katika sehemu ya
mashariki ni wa kujenga njia
tatu za kupleleka umeme za
kaskazini, katikati na kusini.
Njia ya kaskazini ni pamoja
na mifumo ya umeme ya kaskazini
mashariki, kaskazini , Shandong
na kaskazini magharibi, hususan
kuzalisha umeme kwa nguvu
za maji katika sehemu ya kaskazini
magharibi na kupeleka umeme
kwa mifumo ya umeme ya Beijing,
Tianjin,Hebei na Shandong.
Njia ya katikati ni pamoja
na mifumo ya umeme ya sehemu
za mashariki, katikati, Sichuan,
na Fujian, hususan kuzalisha
umeme kwa nguvu za maji ya
mto Changjiang, na kupeleka
umeme kwa sehemu za katikati,
mashariki na Fujian, ambazo
ni sehemu kubwa ya kupelekwa
umeme kutoka sehemu ya magharibi,
na kuleta athari kubwa kwa
mfumo wa umeme wa nchi nzima.
Njia ya kusini ya kupeleka
umeme ni kuzalisha umeme kwa
nguvu za maji za mto Wu ulioko
mkoani Guizhou, mto Lancang
na mto mwekundu ulioko mkoani
Yunnan, pamoja na umeme unaozalishwa
na kiwanda cha umeme cha Kengkou
cha mikoa miwili ya Yunnan
na Guizhou na kupeleka umeme
kwenye sehemu za mkoa wa Guangdong.
Mradi wa kupeleka umeme kutoka
sehemu ya magharibi katika
sehemu ya mashariki ni mradi
mkubwa nchini China, na ni
sehemu muhimu ya mkakati uliotolewa
na serikali ya China wa kustawisha
sehemu ya magharibi, ambayo
inaunganisha rasilimali nyingi
za sehemu ya magharibi na
masoko makubwa ya sehemu ya
mashariki, na itachangia maendeleo
makubwa ya sekta ya uzalishaji
wa umeme na uchumi wa taifa.
|