中国国际广播电台
Sehemu ya magharibi ya China
inaihusisha mikoa 9 ya Gansu,
Guizhou, Ningxia, Qinghai, Shansi,
Sichuan, Tibet, Xinjiang na
Yunnan pamoja na mji wa Chongqing,
ambayo inachukua theluthi mbili
za ardhi na asilimia 22 ya jumla
ya idadi ya watu wa China. Sehemu
ya magharibi ya China ina maliasili
nyingi za madini na hali bora
sana katika nishati ikiwa ni
pamoja na ya nguvu za maji,
utalii na ardhi. Sehemu ya magharibi
ya China, ambayo iko katika
sehemu za juu za mito mingi,
inapakana na nchi zaidi ya 10,
mipaka na nchi jirani ina urefu
wa kilomita 3,500, na kuchukuliwa
kuwa ni ukanda wa pili wa dhahabu
katika ufunguaji mlango kwa
nchi za nje.
Mwaka 2000, utekelezaji wa
ustawishaji wa sehemu ya magharibi
ya China ulizinduliwa, serikali
kuu ilitekeleza sera nafuu
kwa sehemu ya magharibi katika
utengaji wa fedha, mazingira
ya uwekezaji, ufunguaji mlango
kwa ndani na nje, uendelezaji
wa shughuli za sayansi, elimu
na kuvutia watu wenye ujuzi,
na kufanya sehemu hiyo kuwa
ya kuvutia watu katika shughuli
za ustawishaji. Toka mwaka
2000 hadi hivi sasa, China
imeshazindua miradi kadhaa
muhimu ya ujenzi, ambayo fedha
zilizowekezwa zinakaribia
Yuan trilioni 1.
Serikali ya China inabuni
mpango mkuu wa ustawishaji
wa sehemu ya magharibi, na
kutekeleza sera za kuwavutia
wafanyabiashara wa nchi za
nje wawekeze katika sehemu
ya magharibi ya China. Kwa
mfano, serikali ya China imeamua
kutoza kodi ya asilimia 15
ya mapato kwa viwanda vya
wafanyabiashara wa kigeni
vinavyohitajiwa zaidi na China
katika muda wa miaka mitatu
baada ya kupita kipindi cha
utekelezaji wa sera nafuu
zaidi za kodi zinazotekelezwa
hivi sasa, ambapo kwa viwanda
vinavyozalisha bidhaa za kusafirishwa
nchi za nje, kodi ya mapato
inaweza kupunguzwa zaidi hadi
kufikia asilimia 10. Aidha
mikoa na miji ya sehemu ya
magharibi ina haki sawa na
ile ya sehemu ya pwani ambayo
inaweza kuidhinisha bila kibali
cha serikali kuu mradi unaotumia
mitaji ya nchi ya nje wenye
thamani isiyozidi dola za
kimarekani milioni 30. Sasa,
sehemu ya magharibi ya China
imekuwa sehemu mpya ya ufunguaji
mlango kwa nje ambayo inawavutia
zaidi wafanyabiashara wa kigeni.
|