Uhusiano Kati ya China na Marekani

中国国际广播电台

   

 

Mwezi Februari, 1972, rais Richard Nixon wa Marekani alifanya ziara nchini China, ambapo ilitolewa Taarifa ya pamoja ya China na Marekani (yaani “Taarifa ya Shanghai”), ambayo ilionesha kumalizika kwa hali ya kutengana kabisa kati ya China na Marekani kwa zaidi ya miaka 20. Tarehe 16 Desemba, 1978, ilitolewa “Taarifa ya pamoja ya Jamhuri ya watu wa China na Marekani kuwekeana uhusiano wa kibalozi”. Tarehe 1 Januari, 1979, China na Marekani zilianzisha rasmi uhusiano wa kibalozi. Tarehe 17 Agosti 1982, China na Marekani zilitoa “Taarifa ya 8.17” ambayo imeweka kanuni kuhusu Marekani kuiuzia Taiwan silaha, yaani kutatua hatua kwa hatua suala hilo mpaka litatuliwe kabisa.

Mwezi Januari 1984, waziri mkuu wa China Li Peng alifanya ziara nchini Marekani, mwezi Aprili mwaka huo, rais Ronald Reagan alifanya ziara nchini China. Mwezi Julai, 1985, rais Li Xiannia wa China alifanya ziara nchini Marekani. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa rais wa China kuitembelea Marekani.

Mwezi Januari 1998 waziri wa ulinzi wa taifa wa Marekani William Kohen alifanya ziara nchini China, ambapo China na Marekani zilisaini “Mkataba wa wizara za ulinzi wa taifa za China na Marekani kuhusu kuanzisha utaratibu wa kuimarisha mashauriano ya usalama wa kijeshi kwenye bahari”. Tarehe 25,Mei mwaka huo, rais Jiang Zemin na rais Bill Clinton kwa mara ya kwanza walianzisha mawasiliano ya kuongea kwa simu moja kwa moja, siku hiyo walizungumzia hali ya Asia ya kusini na uhusiano kati ya China na Marekani.

Tarehe 25 Juni hadi tarehe 3 Julai mwaka 1998, kutokana na mwaliko wa rais Jiang Zemin, Rais Bill Clinton alifanya ziara nchini China, ambapo marais hao wawili walikuwa na mazungumzo na walikubaliana kuwa China na Marekani zitaimarisha zaidi mazungumzo na ushirikiano kuhusu masuala makubwa ya kimataifa; China na Marekani zimekubaliana kuendelea na juhudi za pamoja na kupiga hatua kubwa kwa lengo la kujenga uhusaino wa kiwenzi na kimkakati unaoelekea karne ya 21. Pande hizo mbili zimeamua kuwa, silaha za nyuklia za kimkakati zinazodhibitiwa na kila upande hazitaulenga upande mwingine; na kukubali kuimarisha zaidi mazungumzo ya kimkakati kwenye sekta za uchumi na fedha ili kutoa mchango mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo mazuri ya uchumi wa dunia na fedha za kimataifa.

Tarehe 1 Januari, 1999, rais Jiang Zemin na rais Clinton walitumiana salamu za kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani. Tarehe 6 hadi 14 Aprili mwaka huo, waziri mkuu wa China Zhu Ronji alifanya ziara rasmi nchini Marekani. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa waziri mkuu wa China kuitembelea Marekani miaka 15 iliyopita.

Tarehe 8 Mei, 1999, saa 11 na dakika 45 ya saa za Beijing, Jumuia ya NATO inayoongozwa na Marekani ilirusha makombora matano kutoka pande tofauti dhidi ya ubalozi wa China nchini Jamhuri ya shirikisho la Yugoslavia, ambapo waandishi watatu wa habari wa China waliuawa, wafanyakazi wengine wa ubalozi huo zaidi ya 20 walijeruhiwa, na jengo la ubalozi huo liliharibiwa vibaya. Wananchi wa China walikuwa na ghadhabu kubwa sana juu ya vitendo hivyo viovu vya Marekani, ambapo uhusiano kati ya China na Marekani uliathiriwa kwa kiasi fulani.

Tarehe 11 Septemba mwaka huo, rais Jiang Zemin na rais Clinton walikuwa na mazungumzo wakati mkutano usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki ulipofanyika huko Aukland, New Zealand, mazungumzo hayo yalipata matokeo yenye juhudi.

Mwaka 2000, mawasiliano kati ya viongozi na ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya China na Marekani uliongezeka. Tarehe 15 Desemba mwaka huo, bunge la Marekani lilipitisha “sheria ya utengaji wa fedha” likafanya mpango wa kufidia dola za kimarekani milioni 2800 kwa hasara za mali za ubalozi wa China nchini Yugoslavia kutokana na mashambalizi ya makombora ya Marekani.

Tarehe 1 Aprili, 2001, ndege moja ya upelelezi wa kijeshi ya aina ya EP-3 ya Marekani ilipofanya upelelezi kwenye anga ya China katika sehemu ya bahari ya umbali wa kilomita 104 toka kusini mashariki ya Kisiwa cha Hainan,China, iligongana na ndege moja ya China iliyoifuata na kuiagusha, ikamfanya rubani wa ndege hiyo ya China Wang Wei kufa papo hapo. Baada ya kuzusha ajali hiyo, ndege hiyo ya Marekani iliingia anga ya mamlaka ya China bila kupata ruhusa, na kutua kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Linshui, kisiwani Hainan, China. Tarehe 11 Aprili, waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Tang Jiashuan alipokea barua ya kuomba radhi kutoka kwa mwakilishi wa serikali ya Marekani ambaye alikuwa balozi wa Marekani nchini China.

Tarehe 11 Septemba mwaka huo, sehemu za New York na Washington za Marekani zilishambuliwa na ugaidi wa kimabavu, na kusababisha vifo na majeruhi wa watu wengi na hasara kubwa za mali. Tarehe 19 Oktoba, rais Jiang Zemin na rais Bush walikutana huko Shanghai, wakibadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani, mapambano dhidi ya ugaidi na masuala mengine makubwa, na walifikia maoni muhimu ya pamoja. Pande hizo mbili zilikubali kwa kauli moja kufanya juhudi za pamoja kwa kuendeleza uhusiano wa ushirikiano wa kiujenzi kati ya China na Marekani.

Mwaka 2002, maendelo ya uhusiano kati ya China na Marekani yalikumbwa na usumbufu kadha wa kadha, lakini kwa ujumla uhusiano huo ulidumisha mwelekeo wa kuboreshwa na kukuzwa. Tarehe 21 hadi 22 Februari, kutokana na mwaliko wa rais Jiang Zemin, rais Bush alifanya ziara nchini China. Marais wa nchi hizo mbili walikutana tena na kujadili kwa kina uhusiano wa pande mbili na hali ya kimataifa, na walikubali kwa kauli moja kuimarisha mazungumzo na ushirikiano kati ya China na Marekani, kushughulikia mwafaka migongano na kufanya juhudi kwa pamoja kusukuma mbele maendeleo ya ushirikiano wa kiujenzi kati ya China na Marekani. Rais Jiang Zemin alipokea mwaliko wa rais Bush, akafanya ziara nchini Marekani mwezi Oktoba kabla ya kwenda Mexico kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki. Rais Jiang Zeming alisisitiza kwa rais Bush kuwa kutatua mwafaka suala la Taiwan kuna umuhimu mkubwa kwa kuendeleza uhusiano kati ya China na Marekani. Rais Bush alisisitiza kuwa Marekani inafuata sera ya kuwepo kwa China moja na kufuata taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, hii ni sera inayofuatwa siku zote na serikali ya Marekani, ambayo haibadiliki.