Uhusiano Kati ya China na Japan

中国国际广播电台

   

 

Tarehe 2 Oktoba, 1971, kisiasa, China ilitoa “kanuni tatu za kurudisha uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan”, yaani Jamhuri ya watu wa China ni serikali pekee halali inayoiwakilisha China; Taiwan ni sehemu moja isiyotengeka ya ardhi ya Jamhuri ya watu wa China; “Mkataba wa amani wa Japan na Chang Keishek” ni haramu ambao hauwezi kufanya kazi, lazima ufutwe. Tarehe 25 Septemba, 1972, waziri mkuu wa Japan Tanaka Kakoei alifanya ziara nchini China, tarehe 29 serikali za China na Japan zilitoa taarifa ya pamoja, na China na Japan ziliufanya uhusiano wa kibalozi uwe wa kawaida.

Hivi sasa uhusiano kati ya China na Japan unadumisha maendeleo kwa ujumla, ambapo matokeo yenye juhudi yamepatikana katika ushirikiano halisi kwenye sekta mbalimbali. Lakini kwa upande mwingine, waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi alikwenda mara kwa mara hekalu kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita, hili limekuwa tatizo kubwa la kuathiri vibaya uhusiano wa kisiasa kati ya China na Japan.

Kiuchumi, China na Japan zimekuwa wenzi wakubwa wa kibiashara. Japan imekuwa mwenzi mkubwa kabisa wa China katika shughuli za biashara kwa miaka mfululizo, na China imekuwa nchi ya pili inayofanya biashara kwa wingi na Japan, ambapo China imekuwa soko kubwa la pili kwa Japan kusafirisha bidhaa nje.

Katika ushirikiano katika sekta za sayansi, elimu, utamaduni na afya, baada ya uhusiano kati ya China na Japan kuwa wa kawaida, pande hizo mbili zimeanzisha ushirikiano wa kiserikali katika mambo ya sayansi na teknolojia, na kusaini “mkataba wa ushirikiano wa kisayansi na kiteknolojia wa China na Japan” mwezi Mei, 1980. Tangu hapo, mawasiliano na ushirikiano wa kisayansi na kiteknolojia kati ya nchi hizo mbili yameendelea kwa haraka na kupanuliwa siku hadi siku kwenye ngazi mbalimbali na kwa aina nyingi.

Tarehe 6 Desemba, 1979, China na Japan zilisaini “Mkataba wa maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na Japan”, kukubali kuendeleza mawasiliano kati ya nchi hizo mbili kwenye sekta za utamaduni, elimu, taalum na michezo. Mwaka 2002 serikali za nchi hizo mbili ziliamua kuanzisha shughuli mbalimbali za maingiliano kama vile “Mwaka wa utamaduni wa China” na “Mwaka wa utamaduni wa Japan”, “Mashindano ya chemsha bongo ya ujuzi kwenye televisheni” na “Baraza la uchumi la China na Japan”.

Hivi sasa kuhusu uhusiano kati ya China na Japan, bado kuna masuala mengi nyeti yanayostahili kushughulikiwa kwa makini:

Kwanza ni suala la kutambua historia. Hili ni suala nyeti la kisiasa katika uhusiano kati ya China na Japan. Tokea mwaka 2001, matukio ya kuchapisha vitabu vya mafunzo ya historia iliyorekebishwa na kupotoshwa na Japan bila kujali ukweli wa mambo ya historia, matukio ya kupotosha historia ya uvamizi wa Japan dhidi ya China, na matukio ya waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi kwenda hekalu kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita yalitokea mara kwa mara, ambayo yamezuia vibaya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Japan.

Pili ni suala la Taiwan. China inashikilia msimamo wazi kuhusu uhusiano kati ya Japan na Taiwan, yaani haipingi mawasialino ya kiraia kati ya Japan na Taiwan, lakini inapinga kithabiti Japan kufanya mawasiliano ya kiserikali ya aina yoyote na Taiwan, kufanya “China mbili” au “China moja, Taiwan moja”, ikiitaka Japan iahidi bayana Taiwan haipo kwenye ushirikiano kati ya Japan na Marekani katika sekta ya usalama.

Tatu ni suala la Visiwa vya Diaoyu. Visiwa vya Diaoyu viko kwenye eneo la bahari ya mashariki yenye maili 92 toka kaskazini mashariki ya mji wa Jilong wa mkoa wa Taiwan wa China, ambavyo viliundwa na visiwa vya Diaoyu, Huangwei, Chiwei, Naixiao na Beixiao pamoja na miamba kadhaa, visiwa hivyo viko karibu sana na Kisiwa cha Taiwan, navyo ni ardhi ya China tangu enzi na dahari, ni sehemu moja isiyotengeka ya ardhi ya China kama Taiwan ilivyo. China inamiliki mamlaka isiyonyimika kwenye visiwa hivyo na eneo la bahari lililo karibu navyo.

Msimamo huo wa China unategemea ushahidi wa kutosha wa kihistoria na kisheria. Mwezi Desemba, 1943, “Taarifa ya Cairo” iliyotolewa na China, Marekani na Uingereza ilieleza kuwa, Japan inapaswa kuirudishia China ardhi ilizoiba kutoka China zikiwa pamoja na sehemu ya kaskazini mashariki ya China, Kisiwa cha Taiwan, na Visiwa vya Penghu. “Tangazo la Potsdam” la mwaka 1945 lilieza kuwa, “sharti lililowekwa kwenye Taarifa ya Cairo lazima litekelezwe”. Mwezi Agosti mwaka huo, Japan ilipokea “Tangazo la Potsdam” na kutangaza kusalimu amri bila masharti, hii imemaanisha kuwa Japan itairudishia China Kisiwa cha Taiwan na Visiwa vya Diaoyu vilivyo karibu nacho.

Nne ni suala la ushirikiano kati ya Japan na Marekani katika sekta ya usalama. Mwaka 1996 Japan na Marekani zilitoa “Taarifa ya pamoja ya ushirikiano wa kiusalama”, kutokana na taarifa hiyo, pande hizo mbili zilianza kurekebisha “Mwongozo wa ushirikiano wa ulinzi” uliotungwa mwaka 1978. Mwezi Septemba, 1997, Japan na Marekani zilithibitisha rasmi mwongozo mpya wa ushirikiano wa kiusalama. Tarehe 24, Mei mwaka 2004, Bunge la Japan lilithibitisha mswada wa sheria unaohusika na mwongozo mpya wa ushirikiano wa kiusalama wa Japan na Marekani, hii imeonesha kuwa utaratibu mpya wa Japan na Marekani katika kuimarisha ushirikiano wa kiusalama umewekwa kimsingi. Juu ya hiyo, China inafuatilia zaidi mwelekeo wake unaohusika na suala la Taiwan, na mwelekeo wake wa kijeshi wa Japan. Mpaka sasa kwa njia mbalimbali China imeeleza ufuatiliaji wake mkubwa na msimamo husika.

Tano ni suala la utoaji fidia wa kivita. Serikali ya Japan ilipofanya mazungumzo na China kuhusu kuufanya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan uwe wa kawaida ilieleza wazi kuwa, imeona inawajibika sana na madhara makubwa kwa wananchi wa China kutokana na vita vyake vya uvamizi, na ilijikosoa kwa makini. Kwa msingi huo, serikali ya China ikizingatia maslahi ya kimsingi ya taifa iliamua kuacha ombi la kufidiwa kutokana na hasasa ilizopata kwenye vita, uamuzi huo uliwekwa kwenye “Taarifa ya pamoja ya China na Japan” iliyosainiwa mwaka 1972. Mwaka 1978, “Mkataba wa amani na urafiki wa China na Japan” ulioidhinishwa kwenye mkutano wa 3 wa bunge la 5 la umma la China ulithibitisha tena kwenye waraka wake wa sheria kuhusu uamuzi wa China wa kuacha kudai fidia kutokana na hasara ilizopata kwenye vita vilivyoanzishwa na Japan.

Sita ni suala kuhusu silaha za kikemikali za Japan zilizoachwa kwenye sehemu ya kaskazini ya China. Wakati wa vita vya kuivamia China, Japan ilifika hadi kukiuka mkataba wa kimataifa, ilitumia silaha za kikemikali na kusababisha vifo na majeruhi wa askari na raia wengi wa China. Jeshi la Japan liliposhindwa katika vita, lilizika na kuacha silaha nyingi za kikemikali katika sehemu lililokalia. Mpaka sasa katika zaidi ya sehemu 30 za mikoa na miji ya China ziligunduliwa silaha hizo zilizoachwa na jeshi la Japan. Katika miaka mingi iliyopita, silaha hizo zimeharibiwa vibaya na kutu, hata zilivuja kila mara, zikaleta tishio kubwa dhidi ya usalama wa maisha na mali za wananchi wa China na mazingira ya viumbe. Serikali ya China ilitoa mashitaka rasmi kwa serikali ya Japan mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, na kuitaka serikali ya Japan itatue suala hilo. Tarehe 30 Julai mwaka 1999, serikali za nchi mbili China na Japan zilisaini “Barua ya kumbukumbu kuhusu kuteketeza silaha za kikemikali zilizoachwa na Japan nchini China”. Katika barua hiyo, serikali ya Japan iliahidi kukumbuka vizuri “Taarifa ya pamoja ya China na Japan” na “Mkataba wa amani na urafiki wa China na Japan”, ikisema imetambua haja ya dharura ya kutatua suala hilo, na kuahidi kutekeleza jukumu lake la kuteketeza silaha hizo kutokana na “Mkataba wa kupiga marufuku silaha za kikemikali”. Hivi sasa idara husika za serikali za China na Japan zikifuata barua ya kumbukumbu zinafanya majadiliano kuhusu namna zitakavyoteketezwa haraka iwezekanavyo silaha zilizoachwa na Japan nchini China.