Umoja wa Asia Kusini Mashariki na China

中国国际广播电台

     

 

Umoja wa nchi za Asia kusini mashariki ulikuwa Umoja wa Asia ya kusini mashariki ulioanzishwa tarehe 31 Julai, 1961. Mwezi Agosit, 1967, nchi tano za Indonesia, Thailand, Singapore, Philippines na Malaysia zilifanya mkutano huko Bangkok na kutoa Taarifa ya Bangkok, zikatangaza kuanzishwa kwa umoja huo. Baadaye nchi tatu za Malaysia, Thailand na Philippines zilifanya mkutano wa mawaziri huko Kuala Lumpur na kuamua kuanzisha Umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki badala ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki.

Nia ya umoja huo:

Kufuata moyo wa usawa na ushirikiano, kufanya juhudi za pamoja kwa kuhimiza ongezeko la uchumi, maendeleo ya jamii na utamaduni ya sehemu hiyo.

Kufuata haki, kanuni za uhusiano kati ya nchi na nchi na “Katiba ya Umoja wa Mataifa”, kuhimiza amani na utulivu wa sehemu hiyo.

Kuhimiza ushirikiano na kusaidiana katika sekta za uchumi, jamii, utamaduni, teknolojia na sayansi.

Kusaidiana katika mambo ya elimu, mafunzo ya kazi na ufundi pamoja na mambo ya utawala na majengo ya utafiti yanayohusika.

Kufanya ushirikaino wenye ufanisi zaidi katika kutumia ipasavyo kilimo na viwanda, kupanua biashara, kuboresha mawasiliano na uchukuzi, na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi.

Kuhimiza utafiti kuhusu masuala ya Asia ya kusini mashariki.

Kudumisha ushirikiano barabara wa kunufaishana na jumuia za kimataifa na kikanda zenye nia na malengo yanayofanana, na kutafuta njia ya kuzidisha zaidi ushirikiano nazo.

Wanachama:

Umoja wa nchi za Asia kusini mashariki una nchi wanachama 10 za Brunei, Cambodia, Indonesia, Laos, Malaysia, Myanmar, Philippines, Singapore, Thailand na Vietnam.

Uhusiano na China:

China imeanzisha uhusiano wa kibalozi na nchi zote wanachama wa Umoja wa Asia kusini mashariki, na mwaka 1996 China imekuwa nchi mwenzi wa umoja huo wa kufanya mazungumzo kwa pande zote.