Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na China

中国国际广播电台

    

 

Mwezi Julai, 2001, marais wa nchi 6 za China, Russia, Kazakstan, Kyrgyzstan, Tajikstan na Uzbekstan walikutana huko Shanghai,China na kusaini “Taarifa ya kuanzishwa kwa Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai”, wakitangaza kuanzisha jumuia mpya ya kikanda ya ushirikiano wa pande nyingi. Nia ya jumuia hiyo ni kuimarisha uaminifu na ujirani mwema na urafiki kati ya nchi wanachama; kuzitia moyo nchi wanachama zifanye ushirikiano wenye ufanisi katika sekta za siasa, uchumi na biashara, sayansi na teknolojia, utamaduni, elimu, nishati, mawasiliano na hifadhi ya mazingira; kufanya juhudi za pamoja katika kulinda amani, usalama na utulivu wa dunia na kanda hiyo; kuanzisha utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi ulio wa kidemokrasia, haki na halali duniani. Pande mbalimbali ziliamua kuanzisha sekretariati ya jumuiya hiyo mjini Beijing.

China ikiwa moja ya nchi zilizopendekeza na kufanya juhudi za kuanzisha Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai, imeshiriki shughuli mbalimbali kwenye jumuia hiyo, kutoa mapendekezo na kanuni nyingi za kiujenzi kwa kuendeleza jumuia hiyo na kutoa mchango mkubwa.