Umoja wa Mataifa na China

中国国际广播电台

   

Umoja wa Mataifa na China

Tarehe 25,Aprili, 1945, wajumbe kutoka nchi 50 walifanya mkutano wa jumuia za kimataifa wa Umoja wa Mataifa. Tarehe 25 Juni, ilipitishwa “Katiba ya Umoja wa Mataifa”. Tarehe 26 Juni, baada ya China, Ufaransa, Urusi, Uingereza, Marekani na nchi nyingi zilizosaini katiba hiyo kukabidhi barua za kuidhinisha katiba hiyo, katiba hiyo ilianza kufanya kazi, na Umoja wa Matafia ulianzishwa rasmi. Mwaka 1947, Baraza kuu la Umoja wa Mataifa liliamua kuwa, tarehe 24 Oktoba iwe siku ya Umoja wa Mataifa.

Nia ya Umoja wa Mataifa ni: Kulinda amani na usalama wa kimataifa; kuendeleza uhusiano wa kirafiki kwenye msingi wa kuheshimu haki za usawa na kanuni za kujiamulia za wananchi wa nchi mbalimbali; kufanya ushirikiano wa kimataifa, ili kutatua masuala ya kimataifa kuhusu uchumi, jamii, utamaduni na ya kibinadamu, na kuhimiza kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kimsingi wa binadamu wote. Ilipofika mwezi Septemba mwaka 2002, Umoja wa Mataifa ulikuwa na nchi wanachama 191, zikiwemo nchi wanachama waanzilishi 49. Makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako New York, Marekani, na ofisi zake nyingine ziko Geneva nchini Uswisi, Vienna nchini Austria, Nairobi nchini Kenya na Bangkok nchini Thailand.

China ni nchi kubwa inayoendelea, pia ni nchi mjumbe wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. China siku zote inashikilia kanuni na kutetea haki katika mambo ya kimataifa, na imekuwa na hadhi muhimu maalum katika Umoja wa Mataifa na jukwaa la kimataifa. Hivi sasa Umoja wa Mataifa unaonesha umuhimu gani katika kusukuma mbele kazi ya kujenga utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi ulio wa haki na halali duniani, hili ni jambo linalofuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Pendekezo la China kuhusu kujenga utaratibu huo, kulinda amani na kusukuma mbele maendeleo na kupinga umwamba linasisitiza usawazishaji na ushirikiano kati ya nchi 5 wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama ili kusaidia amani na maendeleo ya dunia.