Jumuiya ya APEC na China

中国国际广播电台

   

 

Mwezi Januari, 1989, waziri mkuu wa Australia Houk alipoitembelea Korea ya kusini alitoa “pendekezo la Seoul” likishauri kuitisha mkutano wa mawaziri wa sehemu ya Asia na Pasifiki, ili kujadili kuimarisha suala la ushirikiano wa kiuchumi. Baada ya kufanya majadiliano na nchi husika, Australia, Marekani, Japan, Korea ya kusini, New Zealand, Canada na nchi 6 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki zilifanya mkutano wa kwanza wa mawaziri wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi Asia na Pasifiki huko Canberra, mji mkuu wa Australia, tangu hapo Jumuiya ya APEC ikaanzishwa rasmi.

Mkutano wa 3 wa mawaziri wa APEC ulifanyika mwezi Novemba, 1991 na kupitisha “Taarifa ya Seoul”, taarifa hiyo ilithibitisha rasmi nia na lengo la APEC kuwa ni : Kudumisha ongezeko na maendeleo ya uchumi kwa ajili ya maslahi ya pamoja ya wananchi wa sehemu hiyo; kuhimiza uchumi unaosaidiana na kutegemeana kati ya nchi wanachama; kuimarisha utaratibu wa biashara ya pande nyingi na ya ufunguaji mlango; na kupunguza vikwazo vya biashara na uwekezaji wa kikanda.

Jumuiya ya APEC ina nchi 21 wanachama.

Uhusiano kati ya APEC na China

Tangu ijiunge na APEC mwaka 1991, China imefanya juhudi kushiriki katika shughuli mbalimbali za APEC na kuweka mazingira mazuri ya nje kwa mageuzi na ufunguaji mlango wa China, hii pia imesukuma mbele maendeleo kati ya China na nchi wanachama wa APEC. Tokea mwaka 1993, rais wa China kila mwaka huhudhuria mkutano usio rasmi wa viongozi wa APEC, ambapo hutoa mapendekezo na msimamo wa kikanuni wa China, hayo yamechangia mafanikio ya mkutano. Mwaka 2001, China ilifaulu kuendesha mkutano usio wa rasmi wa viongozi wa APEC huko Shanghai, China.