Shirika la biashara duniani WTO na China

中国国际广播电台

   

 

Mwezi Aprili, 1994, mkutano wa mawaziri kuhusu Mkataba mkuu wa biashara forodhani uliofanyika huko Marrakech, Morocco uliamua kuanzisha rasmi Shirika la biashara duniani. Tarehe 1 Januari, 1995, Shirika la biashara duniani WTO lilianzishwa. Nia ya shirika hilo ni kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na biashara ili kuinua kiwango cha maisha, kuhakikisha watu wengi wanapata ajira, kuhakikisha mapato na mahitaji halisi yanaongezeka; kutumia ipasavyo maliasili duniani, kupanua uzalishaji wa bidhaa na kazi ya huduma; kufikia makubaliano ya kunufaishana; kupunguza kwa kiasi kikubwa na kufuta ushuru forodha na kuondoa vikwazo vingine vya kibiashara. Nchi wanachama wa WTO zimefikia 144, na makao makuu yake yako Geneva.

Tokea mwaka 1986 China itoe ombi la kurudisha hadhi ya nchi iliyosaini mkataba mkuu wa biashara forodhani, China imefanya juhudi nyingi kubwa ili kujiunga tena na Shirika la biashara duniani WTO. Tokea mwezi Januari hadi Septemba, 2001, kikundi cha kazi ya China cha WTO kilifanya mkutano mara 4, na kukamilisha mazungumzo ya pande nyingi kuhusu China kujiunga na WTO, pia kupitisha nyaraka za sheria kuhusu China kujiunga na WTO. Tarehe 9 hadi 14 Novemba mwaka huo, mkutano wa 4 wa mawaziri wa WTO ulifanyika huko Doha, Qatar, waziri wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na nje wa China Bwana Shi Guangsheng aliongoza ujumbe kuhudhuria mkutano, ambapo China ilisaini makubalino ya kujiunga na WTO. Tarehe 19 hadi 20 mwaka huo, China ikiwa nchi mwanachama rasmi wa WTO ilihudhuria mkutano wa Baraza kuu la shirika la WTO.