Zhou Enlai

中国国际广播电台



   Zhou Enlai: Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China kuanzia mwaka 1949 hadi 1958.

Zhou Enlai alikuwa mwanamapinduzi, mwanasiasa, mtaalamu wa kijeshi na kidiplomasia wa China, pia alikuwa mmoja kati ya viongozi wakubwa wa Chama cha kikomunisti cha China na Jamhuri ya watu wa China, na mmoja kati ya waanzilishi wa Jeshi la ukombozi wa umma la China. Alizaliwa Huaian mkoani Jiangsu tarehe 5 Machi, 1898, alifariki dunia mwezi Januari, 1976.

Zhou Enlai aliwahi kutunga na kutekeleza sera nyingi za kidiplomasia za China. Mwaka 1954 alihudhuria mkutano wa Geneva. Mkutano huo ulitatua suala la Indo-China, na kuifanya jumuiya ya kimataifa itambue uhuru wa nchi tatu Vietnam (isipokuwa sehemu yake ya kusini), Laos na Cambodia. Zhou Enlai aliiwakilisha China kutetea kanuni za kuishi pamoja kwa amani ichukuliwe kuwa kanuni za uhusiano kati ya nchi na nchi. Mwaka 1955 kwenye mkutano wa Bandung uliofanyika nchini Indonesia, alitetea kuishi pamoja kwa amani, kupinga ukoloni, kutetea kutafuta maoni ya pamoja wakati wa kuweka kando migongano, na kufanya mashauriano kwa kauli moja. Aliwahi kufanya ziara katika nchi kumi kadhaa za Ulaya, Asia na Afrika, aliwahi kuwapokea viongozi na marafiki wengi kutoka nchi mbalimbali duniani, na kuongeza urafiki kati ya wananchi wa China na nchi mbalimbali duniani.