Ji Pengfei

中国国际广播电台


Ji Pengfei: Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China toka mwaka 1972 hadi 1974.

Aliwahi kuwa balozi wa kwanza wa China nchini Ujerumani mashariki, naibu waziri wa mambo ya nje na waziri wa mambo ya nje. Baada ya mwaka 1979, alikuwa mkuu wa idara ya mawasiliano na nje ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, naibu waziri mkuu na katibu mkuu wa baraza la serikali. Alipokuwa mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya Hong Kong na Makau na mjumbe mkurugenzi wa kamati ya utungaji wa mswada wa sheria ya kimsingi ya mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Makau ya Jamhuri ya watu wa China, alitekeleza sera ya serikali ya China ya “nchi moja mifumo miwili” kwa kutatua kiamani masuala ya Hong Kong na Makau, na kuhudhuria sherehe ya kusainiwa kwa taarifa ya pamoja ya China na Uingereza kuhusu suala la Hong Kong.