Huang Hua

中国国际广播电台


Huang Hua : Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China toka mwaka 1976 hadi 1982.

Huang Hua alikuwa mwakilishi wa kudumu wa kwanza wa China katika Umoja wa Mataifa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa tokea China irudishiwe kiti cha halali kwenye Umoja wa Mataifa. Alipokuwa waziri wa mambo ya nje aliwahi kuongoza ujumbe wa China kuhudhuria mkutano wa Baraza kuu la awamu za 29, 32, 33, 35 na 37 la Umoja wa Mataifa. Mwezi Agosti, 1978, hapa Beijing, Huang Hua na waziri wa mambo ya nje wa Japan walisaini “Mkataba wa amani na urafiki wa Jamhuri ya watu wa China na Japan”. Mwaka 1978, aliendesha mazungumzo na mwakilishi wa Marekani kuhusu kuanzisha uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani, na mwaka 1982, Huang Hua na waziri wa mambo ya nje wa Marekani walisaini Taarifa ya tarehe 17, Agosti kuhusu Marekani kuiuzia Taiwan silaha. Hivi sasa bado anashika nyadhifa mbalimbali za jumuiya za China.