MANDHARI NZURI YA KIMAUMBILE 

中国国际广播电台

      
China ina rasilimali nyingi za maumbile, licha ya Jiuzaigou, Zhangjiajie na Huanglong, ambazo zimeorodheshwa kuwa mabaki ya kimaumbile ya dunia, kuna sehemu nyingine zenye mandhari nzuri ya kimaumbile zikiwa ni pamoja na Guilin ya sehemu ya kusini magharibi, milima ya Changbai ya sehemu ya kaskazini mashariki, milima ya Wasichana Wanne ya mkoa wa Guzhou na misitu ya sehemu ya joto ya Xishuangbanna ya mkoa wa Yuannan pamoja na mandhari ya misitu ya minazi ya kisiwa cha Hainan pia ni mandhari nzuri ya kimaumbile.

 MILIMA NA MITO YA GUILIN 


Mji wa Guilin uko katika mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang, kusini magharibi ya China, hali ya hewa ya huko ni ya vuguvugu na yenye unyevunyevu; hakuna baridi kali katika majira ya baridi, wala joto kali katika majira ya joto, na katika majira yote ya mwaka miti na majani huonekana ya rangi ya kijani, wastani wa hali-joto kwa mwaka ni nyuzi 19 za sentigredi.
Guilin ina mazingira bora ya kimaumbile, kutokana na utafiti wa kijiolojia, Guilin ilikuwa bahari kubwa kabla ya miaka milioni 300. kutokana na kuhamahama kwa ardhi ya dunia, mawe ya chokaa yaliyokuwa chini ya maji ya bahari yaliinuka juu na kuwa ardhi, baada ya kupigwa na upepo, jua na mvua kwa miaka mingi, yakawa milima inayopendeza, mapango marefu ya kupendeza na mito iliyopita chini ya ardhi. Sura nzuri ya milima, mto Li, mashamba na vijiji vimekuwa mandhari nzuri ya pekee, ambayo vinajulikana kwa “Mandhari ya Guilin inatia fora duniani”.

 Guilin ni mji wa kale wenye historia ya miaka mingi, ambao uliojengwa miaka 2,110 iliyopita. Hivi sasa, Guilin ina sehemu 109 za hifadhi za vitu vya kali za ngazi za taifa, mkoa na mji. Mashairi yaliyotungwa na wasomi wa enzi mbalimbali ya kusifu milima na mto wa Guilin na sanamu za kibudha, yako katika mapango ya milimani, hususan yako katika Guihai na genge la Mo la mlima wa magharibi. Sehemu maarufu zenye mandhari nzuri katika mji wa Guilin ni pamoja na mlima wa Pilian, bustani ya nyota 7, chemchem ya Longsheng, mawe ya filimbi na mlima wa pua ya ndovu.
Hivi sasa, mji wa Guilin una mahoteli 28 ya ngazi ya nyota ya wageni, mashirika 18 ya utalii na watembelezaji na wakalimani wa lugha za nchi za kigeni wapatao zaidi ya 1,000. Katika miaka ya karibuni, ujenzi wa miundo-mbinu imekuwa ikikamilishwa hatua kwa hatua, hivi sasa kuna njia ya safari za ndege zaidi ya 40 zinazofika kwenye miji mikubwa ya nchi za nje.

MLIMA WA CHANGBAI 


Mlima wa Changbai uko katika mkoa wa Jilin, sehemu ya kaskazini mashariki ya China, ambayo ni mpaka kati ya nchi za China na Korea ya kaskazini na chanzo cha mito mitatu ya Tumen, Yalu na Songhua. Misitu minene isiyo na upeo pamoja na ndege na wanyama adimu wanaoishi ndani yake, imefanya mlima huo kuorodheshwa kuwa hifadhi ya viumbe ya umoja wa mataifa duniani katika mwaka 1980. hivi sasa, mlima wa Zhangbai umethibitishwa kuwa sehemu ya mandhari nzuri ya taifa ya ngazi ya 4A.
Mlima wa Changbai ambao unajulikana kwa “mlima wa kwanza wa sehemu ya kaskazini mashariki”, katika historia ulikuwa sehemu wanayokaa wakazi wa sehemu ya kaskazini mashariki, na pia ni sehemu ya kukua na kustawi kwa kabila la wa-man. Hivyo katika enzi ya Qing, sehemu hiyo ilichukuliwa kuwa ni sehemu takatifu. Mlima wa Changbai unajulikana duniani kwa mandhari nzuri ya utalii, sehemu na kustawi kwa kabila la waman na mlima mtakatifu wa kabila la wakorea.
Mlima wa Changbai unajulikana kwa kuwa na rangi nyeupe kutokana na aina ya mawe meupe ya floatstone na theluji zilizoko katika kilele chake kikuu. Mlima huo ni uliumbwa kutokana na volkano, kutokana na data kuwa mlima huo ulilipukao mara tatu toka karne ya 16. Sura ya ardhi ni nzuri ajabu. Mandhari nzuri za mlima huo ni pamoja na ziwa la mbinguni, misitu ya mbetula, msitu ulioko chini ya ardhi, misonabari warembo, bonde kubwa, bustani iliyoko juu ya mlima, kilele kikuu, chemchem, mlango wa upepo mweusi na msitu wa floatstone.

 Mlima wa Changbai una mazao ya jadi ya gen-seng, ngozi za marten, pembe za paa, licha ya hayo mlimani kuna raslimali za viumbe adimu zikiwa ni pamoja na misonobari warembo, mizabibu na uyoga mwitu, maua ya azelia, chui mkubwa na korongo wenye kichwa mwekundu.
Mawasiliano ya kwenda mlima wa Changbai ni mepesi sana, unaweza kupanda ndege kutoka Beijing, Shanghai na Shenyang hadi mji wa Jianji, halafu kufika huko kwa magari. Kuna mahoteli ya ngazi mbalimbali chini na juu ya mlima, chumba kizuri ni Yuan za Renminbi 220 kwa siku, na kitanda kimoja cha kawaida ni yuan toka 10 hadi 40 kwa siku.