中国国际广播电台
China ni nchi kubwa yenye makabila
mengi, ujenzi wa miji ya sehemu
mbalimbali Una umaalumu wake.
Katika sehemu ya kaskazini ya
China kuna mji mkuu wa Beijing;
sehemu ya mashariki kuna Shanghai,
kitovu cha uchumi wa China;
sehemu ya magharibi kuna mji
wa LahSa wenye umaalumu wa kitibet;
sehemu ya kusini kuna mji wa
Kunming ambao hali ya hewa katika
majira yote manne ya mwaka ni
kama ya Spring. Miji mizuri
iliyoendelea ni kama lulu zinazomeremeta
katika ardhi ya China yenye
kilomita za mraba milioni 9.6.
Hivi Sasa nchini China kuna
miji 137 iliyothibitishwa kuwa
miji bora ya utalii ikiwa ni
pamoja na Shanghai, Beijing,
Tianjin, Chongqing, Shenzhen,
Hangzhou, Dalian, Nanjing, Xiamen,
Guangzhou, Chengdu, Shenyang,
Qingdao, Ningbo, Xian, Haerbin,
Jinan, Changchun na Lasha. Licha
ya hayo China imechagua miji
10 ikiwemo ya Haerbin, Jilin,
Zhengzhou, Zahoqing, Liuzhou
na Qingdao, kuwa miji maarufu
ya kiutamaduni.
BEIJING
Beijing ni mji
mkuu wa China, na ni kitovu
cha siasa na utamaduni nchini
China. Beijing iko katika sehemu
ya kaskazini ya ardhi ya tambarare
ya kaskazini ya China. Kijiografia,
Beijing, Rome ya Italia, Madrid
ya Hispania ziko katika latitudo
moja. Hali ya hewa ya Beijing
ni yenye upepo wa kimajira wa
bara, siku za majira ya baridi
na joto ni nyingi, siku za majira
ya kichipuka na kupukutika ni
kidogo na kukosa mvua. Wastani
wa hali-joto ni nyuzi 11.8 sentigredi
kwa mwaka.
Beijing ina historia ndefu sana
ya kuanzia miaka 3,000 iliyopita.
Katika kipindi cha mwaka 770
hadi mwaka 221 K.K, sehemu ya
Beijing ilikuwa mji mkuu wa
nchi ndogo za himaya ya ufalme,
katika enzi za Qin na Han pamoja
na kipindi cha Nchi Tatu, Beijing
ilikuwa mmoja wa mji muhimu
katika sehemu ya kaskazini ya
China. Beijing ilianza kuwa
mji mkuu wa nchi tangu enzi
ya Jin, ikifuatiwa na enzi za
Yuan, Ming na Qing, ambapo kulikuwa
na wafalme 34 waliotawala dola
kutokea Beijing.
Baada ya kuasisiwa China mpya,
hususan katika miaka zaidi 20
iliyopita baada ya kuanza kutekeleza
sera za mageuzi na ufunguaji
mlango, sura ya Beijing ilikuwa
na mabadiliko makubwa. Majengo
ya kisasa yalijengwa kila mahali
na uhusiano na nchi za nje ulikuzwa
kwa mfululizo. Hivi sasa, Beijing,
inapiga hatua kubwa kuingia
kwenye kundi la miji mikubwa
duniani. Beijing, ambayo mabaki
ya historia yameungana vizuri
na sura ya kisasa, inavutia
watu wa sehemu mbalimbali. Katika
miaka ya karibuni, Beijing kila
mwaka imekuwa inapokea mamilioni
ya watalii kutoka nchi za nje
na milioni ya makumi ya watalii
wa nchini.
Historia ndefu iliiachia Beijing
vitu vingi vya kale pamoja na
utamaduni murua wa jadi. Ikiwa
unapenda vitu na mabaki ya utamaduni,
unaweza kwenda kuona Ukuta Mkuu,
kutembelea makasri makubwa,
au kutembelea bustani za kifalme
ambazo ni pamoja na Summer Palace,
Beihai, Xiangshan na Tiantan.
Mandhari nzuri na majengo makubwa
ya huko yatafanya wewe kutoka
kuondoka. Ikiwa unataka kufahamu
utamaduni na mambo kuhusu watu
mashuhuri wa China, unaweza
kutembelea maskani mengi ya
watu mashuhuri au kwenda kusikiliza
Beijing opera. Ikiwa unataka
kujua hali ya maendeleo ya maeneo
mbalimbali ya siasa, uchumi,
sayansi na teknolojia na kijeshi,
unaweza kwenda kutembelea majumba
ya makumbusho zaidi ya mia moja
yaliyoko mjini Beijing. Ukitaka
kujiburudisha kwa mandhari nzuri
ya kimaumbile ya Beijing, unaweza
kwenda kuangalia milima na mito
iliyoko katika sehemu ya mzunguko
wa Beijing.
Hivi sasa, sehemu za mandhari
ya ngazi ya 4A zilizoko hapa
Beijing ni pamoja na Tiantan,
makaburi 13 ya enzi ya Ming,
Summer Palace, Jumba la wanyama
wa baharini la Beijing, Ukuta
Mkuu wa Badaling, Mlima wa Jing,
Bustan ya Beihai, bustani ya
makabila ya China, Jumba la
sayansi na teknolojia la China,
bustani ya wanyama la Beijing
na Bustani ya mimea ya Beijing.
XIAN
Xian, ambayo iko katika sehemu
ya kaskazini magharibi ya China,
ni mji mkuu wa mkoa wa Shanxi
na kuchukuliwa kuwa ni kitovu
cha siasa, uchumi na mawasiliano
cha sehemu ya kaskazini magharibi
na China bara.
Mji wa Xian ni mmoja kati ya
miji sita ya kale ya China ambayo
ni Xian, Luoyang, Nanjing, Kaifeng,
Hangzhou na Beijing. Xian ni
mji mkuu wa enzi nyingi na kwa
muda mrefu zaidi kuliko miji
mingine ya kale, na kujulikana
sana kwa historia na utamaduni
wake. Katika historia ya China,
wataalam wa elimu ya historia
wamethibitisha kuwa enzi 10
za Zhou ya magharibi, Qin, Han
ya magharibi, Zhao ya awali,
Qin ya baadaye, Wei ya magharibi,
Zhou ya kaskazini, Sui na Tang
zilichagua Xian kuwa ni mji
mkuu. Hivyo, mji wa Xian wenye
historia ya zaidi ya miaka elfu
moja, una athari kubwa katika
historia na ni wa kipekee ukilinganishwa
na miji mingine.
Xian, ambao unachukuliwa kuwa
ni mmoja kati ya miji minne
ya kale duniani, ni sehemu maarufu
ya utalii. Sanamu za askari
na farasi wa mfalme Qingshihuang,
ambazo zinasifiwa kuwa ni “ajabu
kubwa la nane duniani” ziko
katika wilaya ya Lintong ya
mji wa Xian, sanamu za askari
na farasi ni zaidi ya 6,000
kwa jumla, na kuchukuliwa kuwa
ni ugunduzi mkubwa kabisa wa
karne ya 20. Licha ya hayo kuna
sehemu nyingine za mandhari
nzuri zikiwa ni pamoja na Mnara
wa Wide Goose, Dimbwi la Huaqing,
na mlima wa Hua. Picha hiyo
ni Ukumbi wa makumbusho ya sanamu
za askari na farasi za mfalme
Qinshihuang.
LAHSA
Lahsa
ni mji mkuu wa mkoa unaojiendesha
wa Tibet, China, ambao uko
katika upande wa kaskazini
wa mlima wa Himalaya, eneo
lake ni kilomita za mraba
29,052. hali ya hewa ya Lahsa
ni ya uwanda wa juu, kuna
siku nyingi zenye jua, mvua
kidogo, hakuna baridi kali
katika majira ya baridi wala
joto kali katika majira ya
joto, wastani halijoto katika
mwaka ni sentigredi nyuzi
7.4; Mvua hunyesha katika
miezi mitatu ya 7, 8 na 9,
na kiwango cha mvua ni kiasi
cha milimita 500; Jua linawaka
kwa saa zaidi ya 3,000 kwa
mwaka, hivyo Lahsa unajulikana
kuwa ni “mji wa mwangaza”.
Lahsa ina hewa safi, jua nzuri,
mchana ni joto kiasi na usiku
ni baridi, hivyo ni sehemu
nzuri sana ya kukwepa joto
kali katika majira ya joto.
Lahsa iko katika uwanda wa
juu wa Qinghai na Tibet, ambao
unajulikana kama “paa la dunia”,
uko katika wastani wa mita
3,600 juu ya usawa wa bahari,
hakuna hewa ya oxygen ya kutosha,
ina upungufu wa hewa hiyo
kwa kati ya 25% hadi 30% ikilinganishwa
na sehemu nyingine za China
bara. Katika siku za mwanzoni
watu husikia maumivu ya kichwa
na kupumua kwa haraka. Katika
siku ya kwanza baada ya kufika
Lahsa, mtu anapaswa kupumzika
ili kuzoea hali ya huko. Kipindi
cha kati ya mwezi Aprili na
Oktoba ni kizuri kwa utalii
huko Tibet. Katika lugha ya
Kitibet, Lahsa ni mahali patakatifu
anapokaa mungu. Mji wa Lahsa
umekuwa na historia ndefu
na jadi ya kidini, sehemu
za utalii mjini ni pamoja
na hekalu ya Dazhao, mtaa
wa Baguo na kasri la Budala.
(picha
hiyo ni kasri la Budala ya
Lahsa)
|