中国国际广播电台
Miji ya China ina historia ndefu,
hususan baadhi ya miji midogo
iliyojengwa zaidi ya miaka mia
moja iliyopita, inavutia watu
zaidi, kwa mfano, mto Li wa
mkoa wa Yunnan umeorodheshwa
kuwa ni urithi wa utamaduni
duniani. Historia na utamaduni
wa miji midogo pamoja na siku
za jana na leo zimeanza kutembelewa
na watalii wa nchini na wa nchi
za nje.
TARAFA YA ZHOUZHUANG
Tarafa
ya Zhouzhuang iko katika mkoa
wa Jiangsu, sehemu ya mashariki
ya China, umbali wa kilomita
38 tu kutoka mji wa kale wa
Suzhou. Mchoraji mashuhuri wa
michoro ya kichina Bw. Wu Guanzhong
aliwahi kuandika makala ikisema
kuwa Mlima Manjano umekusanya
uzuri wa milima ya China, na
tarafa ya Zhouzhuang imekusanya
uzuri wa vijiji vyenye mito
na maziwa”, magazeti ya nchi
za nje yanasifu Zhouzhuang kuwa
ni “tarafa ya kwanza yenye mito
na maziwa nchini China”.
Tarafa ya Zhouzhuang inazungukwa
na maziwa ya Deng, Baiyan, Dingshan,
na Nan pamoja na mito ya wastani
na midogo zaidi ya 30, nyumba
za wakazi zote zimejengwa kando
ya mito, ambazo ni nyumba za
mtindo wa kale na zenye ua.
Zaidi ya 60% nyumba za tarafa
hiyo zilijengwa katika enzi
za Ming na Qing, tarafa hiyo
ya kale yenye kilomita ya mraba
0.4, ina nyumba za mtindo wa
kale karibu 100, pamoja na malango
makubwa zaidi ya 60 yaliyojengwa
kwa matofali. Licha ya hayo,
tarafa ya Zhouzhuang imehifadhi
vizuri madaraja 14 yenye utaalamu
wa kale, mandhari ambayo ni
kama watu wanavyosema kuwa “madaraja
madogo, mito na nyumba za wakazi”.
Mazingira ya Zhouzhuang ni mazuri
na hayana makelele, hivyo ni
sehemu nzuri za kusoma, wenyeji
wa huko wana jadi ya kusoma,
katika historia walijitokeza
wasomi wakubwa zaidi ya 20.
Wasomi na washairi wengi kutoka
sehemu nyingine walitunga mashairi
na kuchora michoro juu ya uzuri
wa tarafa hiyo. Mfasihi wa enzi
ya Jin ya magharibi Zahng Han,
washairi wa enzi ya Tang Li
Yuxi na Lu Guimeng waliwahi
kukaa katika tarafa ya Zhou.
Mandhari muhimu ya tarafa
ya Zhou ni pamoja na hekalu
la Quanfu, chuo cha dini ya
Dao cha Chengxu, Ukumbi wa
Shen, daraja la Fuan na Jumba
la mi. Tarafa ya Zhou iko
katikati ya Suzhou na Shanghai,
mawasiliano ni mepesi sana,
kuna mabasi yanayofika huko
moja kwa moja. Kwa kuwa Zhouzhuang
iko karibu na Shanghai, hivyo,
watalii wanaweza kwenda na
kurudi kwa siku moja, huko
hakuna mahoteli mengi ya ngazi
ya nyota, lakini nyumba za
kawaida za wageni ni nyingi,
ingawa nyumba hizo siyo za
hali ya juu, lakini ni safi
sana.
MJI WA KALE WA PHOEINIX
Tarafa ya Phoenix iko katika
wilaya inayojiendesha ya makabila
ya watuju na wamiao, sehemu
ya magharibi ya mkoa wa Hunan,
katikati ya China.“Mji wa
kale wa Phoeinix” unaoitwa
na mwandishi wa vitabu wa
New Zealand Luis Ari kuwa
ni mmoja wa mji mdogo nzuri
kabisa nchini China, ulijengwa
katika nasaba ya Kangxi ya
enzi ya Qing. Mji huo unaojulikana
kwa “Lulu ya magharibi ya
mkoa wa Hunan” ni mdogo kweli
kweli, na kuna barabara moja
tu mjini humo.
Mji wa kale wa Phoenix una
sehemu mbili za mji wa kale
na mji mpya, mji wa kale uko
kando ya mto, chini ya mlima,
mto Tuo unapita katikati ya
mji, ukuta mrefu wa mji ulijengwa
kwa mawe mekundu kando ya
mto, na mlima wa Nanhua uko
karibu na mji wa kale. Ngome
ya mji ulijengwa katika enzi
ya Qing. Katika mto mpana
ulioko karibu sana na mlango
mkubwa wa kaskazini wa mji,
lilijengwa daraja moja jembamba,
watu wawili wakikutana kwenye
daraja hilo, hawana budi kugeuza
miili yao ili mmoja kumpisha
mwenzie. Daraja hilo lilikuwa
daraja pekee la kutokea nje
kwa wakazi wa mji huo.
Tarafa ya Phoenix imejulikana
kutokana na kuwa ni maskani
ya mwanzo kabisa ya mwandishi
vitabu mashuhuri Shen Congwen
wa miaka ya karibuni. Maskani
ya mwandishi vitabu huyo alikaa
ndani sana ya kichochoro kimoja
kilichotandikwa vipande vya
mawe kwenye mtaa wa Ying wa
mji huo wa kale. Nyumba yake
ilijengwa kwa matofali na
mbao ni kama nyumba ya kijadi
ya Beijing. Sehemu muhimu
ya mandhari ya tarafa ya Phoenix
ni pamoja na kuangalia jua
likichomoza katika mlima wa
mashariki, misitu ya mlima
wa Nanhua, makengele yakilia
katika hekalu iliyojengwa
mlimani, mashua za wavuvi
zenye kandili katika usiku
na kuangalia mbalamwezi kwenye
daraja na Xi. Watalii wanaweza
kuwasili mji wa Jishou mkoani
Hunan kwa ndege kisha kutumia
mabasi.
|