HALI YA VITOWEO VYA CHINA

中国国际广播电台

      
Vitoweo vya China vimegawanyika katika aina nane kutokana na umaalumu wa mapishi yake, zikiwa ni pamoja na Shandong, Sichuan, Guangdong, Fujian, Jiangsu, Zhejiang, Hunan na Anhui.
Kukamilika kwa aina moja ya vitoweo kunahitaji miaka mingi na umaalumu wa mapishi yake, vilevile kunaathiriwa na hali za kijiografia, hewa, rasilimali na mazoea ya chakula. Kulikuwa na mtu aliyefananisha mapishi ya vitoweo ya Jiangsu na Zhejiang kama warembo wembamba wa sehemu ya kusini ya China; Vitoweo vya mikoa ya Shandong na Anhui kama watu makamo wenye nguvu wa sehemu ya kaskazini; vitoweo vya mikoa ya Guangdong na Fujian kama vijana watanashati; Na vitoweo vya mikoa ya Sichuan na Hunan kama wasomi wenye ujuzi na elimu nyingi.