Vitoweo vya Shandong
Vitoweo vya mkoa wa Shandong
ni pamoja na vya sehemu
mbili za kusini mwa mji
wa Jinan na mashariki ya
Shandong. Umaalumu wake
ni kuwa na chumvi na mafuta
mengi, vikichanganywa na
vitunguu na vitunguu saumu.
Vitoweo vizuri vya aina
hiyo ni pamoja na vyakula
vya baharini, supu na maini
na utumbo wa wanyama.
Vitoweo vya Sichuan
Vitoweo vya Sichuan ni pamoja
na vya miji miwili ya Chenngdu
na Chongqing. Umaalumu wake
ni vyenye ladha, chumvi
na pili nyingi. Vitoweo
vinavyopendwa sana na watu
ni pamoja na vipande vidogo
vya nyama ya kuku vinavyokaangwa
pamoja na karanga na pilipili,
viganja vya dubu, vipande
vya nyama ya nguruwe pamoja
na pilipili, mapezi ya papa
na kaa wa baharini;
(图:香辣炒蟹)
Vitoweo vya Jiangsu
Vitoweo vya Jiangsu ni vya
miji ya Yangzhou, Suzhou
na Nanjing.
Umaalumu wa vitoweo hivyo
ni kuzingatia kutumia viungo
na kuhifadhi mchuzi wake
wa asili. Mbinu zinazotumika
katika mapishi ni kuchemsha.
Vitoweo vyake maarufu ni
vipande vidogo vidogo vya
nyama na mboga vilivyopikwa
kwa kutumia supu ya kuku,
na makongoro ya nguruwe
yaliyochanganywa na unga
wa nyama ya kaa wa baharini.
Vitoweo vya Zhejiang
Vitoweo vya Zhejiang ni
pamoja na miji ya Huangzhou,
Ningbo na Shaoxing, ambavyo
vya Hangzhou vinajulikana
zaidi.
Umaalumu wa vyakula hivyo
ni laini, vyenye ladha nzuri
na kutokuwa na mafuta mengi.
Vitoweo maarufu ni kamba
wadogo wa baharini wenye
harufu ya chai, kuku pamoja
na samaki wenye ladha ya
siki.
Vitoweo vya Guangdong
Vitoweo vya Guangdong ni
pamoja na vya miji Guangzhou,
Chaozhou, na Dongjiang,
ambavyo vya Guangzhou ni
vyenye sifa kubwa zaidi.
Umaalumu wa vitoweo hivyo
ni vyenye ladha nzuri na
kutumia chumvi kidogo sana.
Vitoweo maarufu ni pamoja
na nyama za aina tatu za
nyoka, paka na kuku, nguruwe
mchanga mzima, aina ya tikiti
maji nyeupe, na nyama ya
Gulao.
Vitoweo vya Hunan
Vitoweo vya Hunan vinazingatia
ladha nzito za pilipili
na siki. Na vitoweo maarufu
ni pamoja na mbegu za yungiyungi
tamu na mapezi ya papa
Vitoweo vya Fujian
Vitoweo vya Fujian ni vya
miji ya Fuzhou, Quanzhou
na Xiamen, ambavyo vya mji
wa Fuzhou ni maarufu zaidi.
Umaalumu wa wake ni kutumia
vyakula vya bahairni, na
kuzingatia ladha tamu, siki
na chumvi.
Vitoweo maarufu ni pamoja
na kuku, samaki mwenye maji
ya machenza, kamba wa Taiji
na samaki waliokaangwa.
Vitoweo vya Anhui
Vitoweo vya Anhui ni pamoja
na vya sehemu ya kusini
ya Anhui na sehemu za kando
mbili za mto Changjiang
na Huai. Vitoweo vya sehemu
ya kusini ya Anhui ni maarufu
zaidi.
Umaalumu wa vitoweo hivyo
ni kuongeza ladha ya vitoweo
kwa ham, sukari na kwa mbinu
ya kuchemsha kwa moto mkubwa
na mdogo.
Vitoweo maarufu ni pamoja
na nyama ya mabata yaliyochanganywa
na mbuyu na kuku.