中国国际广播电台
Kati ya vitoweo vya maeneo
maalumu manane, vitoweo vya
mkoa wa Sichuan vimeenea katika
sehemu nyingi zaidi.
Vitoweo vya Sichuan vinajulikana
kwa miaka mingi, na vimewavutia
watu wa nchini na wa nchi
za nje kwa sifa yake ya kipekee.
Vitoweo vya Sichuan vinazingatia
rangi, harufu, namna vinavyoonekana
na hususan ladha yake, na
kutumia ipasavyo viungo vya
aina mbalimbali.
Pamoja na maendeleo ya uzalishaji
mali na ustawi wa uchumi,
juu ya msingi wake wa asili,
vitoweo vya Sichuan vina sifa
za vitoweo vya sehemu za kusini
na kaskazini pamoja na ubora
wa vitoweo vya karamu ya kuribisha
wageni. Hivi sasa vitoweo
vya Sichuan vimekuwa na sifa
kubwa, ambayo watu wanasema,
“Chakula kizuri kiko China,
Vitoweo vitamu viko Sichuan”.
Vitoweo vya Sichuan vinatia
maanani mabadiliko ya ladha,
ambavyo hakuna kitoweo kinachokosa
viungo vya aina tatu muhimu,
yaani pilipili, mbegu za Bunge
prickly ash na pilipili manga.
|