中国国际广播电台
Mgeni anapopita kwenye
forodha ya China anatakiwa
kufuata maagizo husika ya
forodha ya China, ili kufanikisha
matembezi yako na kupita kwenye
forodha bila matatizo, anatakiwa
kufahamu mambo yafuatayo:
Mtalii anaondoka China akichukua
au kusafirisha vitu vinavyo
orodheshwa hapo chini, anatakiwa
kuieleza forodha:
Vitu vinavyotozwa ushuru,
na kiasi cha vitu vinavyoingia
nchini bila kulipa ushuru
Vitu vinavyotumiwa na wasafiri
wenyewe safarini pamoja na
vitu ambavyo haviko katika
eneo la vitu vinavyotumiwa
na wasafiri wenyewe safarini,
lakini bado vinahesabiwa kuwa
ni vitu wanavyohitaji safarini;
Vitu vinavyopigwa marufuku
kuingia au kutoka China pamoja
na kiasi cha vitu vinavyoruhusiwa
kuingia na kutoka China vikiwa
ni pamoja na vitu vya kale,
sarafu, dhahabu, fedha pamoja
na vitu vilivyotengenezwa
kwa madini hayo, maandishi
yaliyochapishwa, na kaseti
za audio na video;
Bidhaa, sampuli za bidhaa
na vitu ambavyo haviko katika
eneo la mizigo ya watalii.
NJIA ZA RANGI NYEKUNDU
NA KIJANI
Wasafiri wanaotakiwa kulipa
ushuru na wale waliohitaji
kibali kwa mizigo yao wapite
kwenye “njia nyekundu”; wasafiri
wengine wanaweza kupita kwenye
“njia ya rangi ya kijani”.
KANUNI ZA KAWAIDA
Kwa kawaida, msafiri anapopita
kwenye forodha, mizigo yote
aliyokuwa nayo inatakiwa kukaguliwa.
Mizigo ambayo haijakubaliwa
na forodha haichukuliwi au
kusafirishwa.
Mizigo yake iliyosafirishwa,
ambayo haikuwa pamoja na msafiri
inatakiwa kutolewa maelezo
katika “fomu ya mizigo ya
msafiri”, na inatakiwa kuingia
au kutoka nchini katika muda
wa miezi 6 baada ya msafiri
kuingia au kutoka China.
“Fomu ya mizigo ya msafiri”
iliyosainiwa na mfanyakazi
wa forodha inatakiwa kutunzwa
vizuri ili ashughulikiwe haraka
wakati atakapoondoka au kuingia
nchini.
Aidha, msafiri anapaswa kutoa
maelezo kwa forodha wakati
anapoondoka China akichukua
vitu vya mabaki ya kiutamaduni.
Vitu vya mabaki ya kiutamaduni
alivyonunua msafiri katika
maduka yenye leseni ya biashara
ya mabaki ya kiutamaduni,
forodha inamruhusu kuondoka
baada ya kukagua risiti maalumu
za biashara hiyo yenye muhuri
wa idara ya usimamizi wa mabaki
ya kiutamaduni ya China. Msafiri
akitaka kuondoka nchini na
kuchukua vitu vya mabaki ya
kiutamaduni ambavyo alivipata
kwa njia nyingine vikiwa ni
pamoja na kurithi kutoka wazazi
au kupewa zawadi na marafiki,
anapaswa kuthibitishwa na
idara ya usimamizi wa vitu
vya mabaki ya kiutamaduni
ya China. Hivi sasa, idara
hiyo imefungua ofisi zake
katika forodha za miji minane
ikiwemo ya Beijing, Shanghai,
Tianjin na Guangzhou. Vitu
vinavyoruhusiwa kuchukuliwa
katika nchi za nje baada ya
kuthibitishwa na kupewa kibali
na idara ya usimamizi wa mabaki
ya vitu vya kiutamaduni vinakubaliwa
kupita kwenye forodha ya China.
|