Idara ya karantini ya China
ni idara ya utekelezaji wa sheria
iliyoanzishwa kutokana na agizo
la serikali kuhusu shughuli
za karantini zinaohusika na
nchi za nje, idara hiyo na vitengo
vilivyo chini yake katika forodha
zilizofunguliwa mlango kwa nchi
za nje kufanya ukaguzi wa karantini
kwa mujibu wa sheria juu ya
watu wanaoingia na kutoka nchini,
na forodha zinatoa ruhusa ya
kuingia au baada ya kuona vyeti
vilivyosainiwa na vitengo vya
karantini.
Vyombo vya mawasiliano, watu,
chakula, maji ya kunywa pamoja
na wadudu na maradhi ya kuambukiza
vinafuatiliwa zaidi.
Vitengo vya karantini vinawazuia
wageni wenye baadhi ya magonjwa
kuingia nchini, ambao ni pamoja
na wenye virusi vya ukimwi,
magonjwa ya zinaa ya kuambukiza
na kifua kikuu kilichoko katika
kipindi cha kuambukiza.