Makabila ya China

Radio China Kimataifa

China ni nchi yenye makabila mengi, ina idadi kubwa kabisa ya watu duniani. Hivi sasa China ina watu bilioni 1.3 na makabila 56.

Makabila ya China ni kama yafuatayo: wahan, wamongolia, wahui, watibet, wauigur, wamiao, wayi, wazhuang, wabuyi, wakorea, waman, watong, wayao, wabai, watujia, wahani, wakazakstan, wadai, wali, walisu, wa-wa, washe, wagaoshan, walahu, washui, wadongxiang, wanaxi, wajingpo, wakhalkhas, wa-tu, wadawoer, wamulam, waqiang, wabulang, washala, wamaonan, wagelao, waxibo, waachang, wapumi, watajik, wa-nu, wauzbek, warussia, waewenk, wadeang, wabaoan, wayugu, wajing, watataer, wadulong, waelunchun, wahezhe, wamenba, waluoba na wakinuo. Zaidi ya hayo, nchini China pia kuna watu wasiojulikana wa kabila gani.

Nchini China, watu wa kabila la Han wanachukua takriban asilimia 92 ya idadi ya wachina wote, ambapo watu kutoka kwenye makabila madogo 55 wanachukua asilimia 8. Kwa kuwa idadi ya watu wa makabila mengine 55 ni ndogo , hivyo huitwa makabila madogo. Makabila mengi madogo yanakaa katika sehemu ya kaskazini magharibi, kusini magharibi na kaskazini mashariki mwa China.

Kutokana na maendeleo ya historia ndefu ya China, watu wa kabila la Han na baadhi ya makabila madogo wanaishi kwa kuchanganyika,ambapo watu wengine wa makabila madogo wanakaa katika sehemu ndogo. Licha ya kabila la Hui na kabila la Man yanayotumia lugha ya Han, yaani lugha ya taifa la China, makabila mengine madogo yote yana lugha zao zenyewe huku wakitumialugha ya Kichina. Katika miaka mingi iliyopita, watu wa makabila 56 wa China walikuwa wakifanya kazi na kuishi pamoja kwenye eneo lenye kilomita za mraba milioni 9.6, na kukuza kwa pamoja ustaarabu wenye historia ndefu.