Makabila Yenye Watu Zaidi ya Milioni Tano

Radio China Kimataifa

Kabila la Han

Kabila la Han ni kabila lenye idadi kubwa kabisa la watu nchini China hata duniani. Hivi sasa lina watu bilioni 1.2. Watu wa kabila la Han walikuwa wakazi wa sehemu ya katikati ya China, ambao waliitwa "huaxia", wamekuwa na ustaarabu wenye historia ya miaka 5000. Baadaye waliishi pamoja na makabila mengine. Kuanzia enzi ya Han, watu wa "huaxia" walianza kuitwa rasmi kuwa kabila la "Han", lilikuwa na lugha na maandishi yake yenyewe, yaani Kichina. Kichina ni lugha ya mfumo wa "Han-Tibet", hugawanyika kuwa lahaja aina nane za kienyeji, yaani kaskazini, Wu, Xiang, Gan, Kejia, Minnan, Minbei na Yue. Kichina sanifu pia kinaitwa "Mandrine", Kichina ni moja ya lugha zenye historia ndefu zaidi duniani, maandishi yake yaliendeleza taratibu kutoka maandishi yaliyoandikwa kwenye mifupa au magamba ya kobe, au shaba nyeusi hadi herufi za Kichina za sasa (Chinese characters), Kichina kina maneno zaidi ya elfu 80, kati yao maneno 7000 yanatumika mara kwa mara. Hivi sasa Kichina ni moja ya lugha za kimataifa zinazotumiwa na watu wengi.

 Watu wa kabila la Han wanapenda kula chakula cha nafaka, nyama na mboga. Tangu zamani sana, watu wa kabila la Han wamekuwa na desturi ya kula mara tatu kila siku. Vyakula vya mchele na unga wa ngano ni aina muhimu kwa wa-Han. Zaidi ya hayo, nafaka nyingine kama vile mahindi, mtama na viazi pia hutumiwa na wa-han katika sehemu tofauti. Kutokana na mila na desturi mbalimbali, watu wa kabila la Han katika sehemu tofauti wanakula vyakula vyenye ladha tofauti, kwa mfano watu wa kusini wanapenda vyakula vyenye sukari, watu wa kaskazini wanapenda vyakula vyenye chumvi chumvi nyingi zaidi, watu wa mashariki wanapenda kula vyakula vyenye pilipili na watu wa magharibi wanapenda vyakula vya tindikali. Hivi sasa, China ina aina nane kuu za vitoweo vyenye ladha tofauti.

Pombe na chai ni vinywaji viwili vikuu vya kabila la Han. China ni maskani ya chai, pia ni moja ya nchi zilizovumbua ufundi wa kutengeneza pombe mapema zaidi duniani, utamaduni wa pombe na chai wa China ni wenye historia ndefu. Licha ya pombe na chai, vinywaji vilivyotengenezwa na matunda pia vinapendwa sana na watu wa Han.

Watu wa Han wana sikukuu nyingi, sikukuu ya spring ya mwaka mpya ni sikukuu muhimu kabisa kwa kabila la Han. Zaidi ya hayo, sikukuu nyingine muhimu ni kama sikukuu ya taa (lantern festival) katika tarehe 15 Januari ya mwaka wa kijadi, siku ya Qingming ya kusafisha makaburi (Tomb-sweeping Day) ya tarehe 5 Aprili, sikukuu ya "dragon boat festival" ya tarehe 5 Mei na sikukuu ya "mid-autumn festiva" ya tarehe 15 Agosti, sikukuu hizo huwekwa katika kalenda ya kichina.

Wazhuang  

Kabila la Zhuang ni kabila lenye idadi kubwa zaidi la watu kulingana na makabila madogo madogo mengine nchini China. Watu wa kabila la Zhuang wanaishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Zhuang wa Guangxi, kusini mwa China, wanatumia lugha ya kizhuang, ambayo ni lahaja ya mfumo wa lugha wa Han-Tibet. Watu wa Zhuang ni wenyeji wa kusini mwa China, wana historia ndefu. Zaidi ya miaka elfu makumi iliyopita, wahenga wa Zhuang waliishi katika sehemu hiyo. Mkoa unaojiendesha wa kabila la Zhuang wa Guangxi ulianzishwa mwaka 1958.

Watu wa kabila la Zhuang wanajishughulisha na kilimo, hasa kilimo cha mpunga na mahindi. Watu wa Zhuang wanapenda kuimba, hivyo maskani ya kabila la Zhuang husifiwa kuwa "bahari ya nyimbo". Nguo za tarizi ni sanaa za mikono za kijadi za watu wa Zhuang. Watu wa Zhuang zamani walikuwa waumini wa dini ya kiasili ambao waliabudu maumbile na miungu wengi. Baada ya enzi ya Tang na Song, dini za Buddha na Tao zilienezwa hadi sehemu walikoishi watu wa Zhuang. Katika enzi ya hivi karibuni, dini ya kikristo pia zimeingizwa katika sehemu ya Zhuang, lakini haina athari kubwa.

 


Kabila la Man  

Watu wa kabila la Man wanaishi kote nchini China, lakini wengi wao wanaishi katika mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki ya China. Watu wa kabila la Man walizungumza Kiman, ni lugha ya mfumo wa Altai. Baada ya kuishi pamoja na watu wahan, hivi sasa watu wengi wa Man wanatumia Kichina, ni wazee wachache tu wanaoishi katika vijiji vya pembezoni wanaweza kuzungumza lugha ya Kiman. Watu wa Man waliwahi kuamini dini ya Shaman yenye miungu wengi. Kabila la Man lina historia ya miaka zaidi ya 2000. Wahenga wao siku zote waliishi katika sehemu ya mtiririko wa kati na chini wa mto Heilongjiang na mtiririko wa mto Wusuli, kaskazini ya mlima wa Changbaishan, kaskazini mashariki mwa China. Katika karne ya 12, kabila la Man lililoitwa "Nuzhen", lilianzisha enzi ya Jin. Mwaka 1583 Nuerhachi aliunganisha makundi mbalimbali ya "Nuzhen", kuanzisha mfumo wa "Bendera Nane" za kabila la Man, na kuanzisha lugha ya Kiman, na kulipa kabila hilo jina la "Manzhou" mwaka 1635. Mwaka 1636, Nuerhachi akawa mfalme, na kuanzisha enzi ya Qing. Mwaka 1644, jeshi la enzi ya Qing lilisonga kusini na kuiangusha enzi ya Ming. Enzi ya Qing ilikuwa enzi kifalme ya mwisho ya ya China iliyo chini ya utawala wa serikali kuu. Baada ya mapinduzi ya Xinhai, kabila hilo lilianza kuitwa rasmi kuwa kabila la Man. Watu wa Man walitoa mchango mkubwa kwa umoja, upanuaji wa ardhi na maendeleo ya uchumi na utamaduni wa China.



Kabila la Hui

Kabila la Hui lina idadi ya watu zaidi ya milioni 9.8, wengi wao wanaishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Hui wa Ningxia, kaskazini magharibi mwa China. Baadhi yao wanasambaa katika sehemu mbalimbali, ni kabila dogo linaloenea katika sehemu nyingi sana za China. Watu wa Hui wameishi pamoja na watu wa Han kwa kipindi kirefu, hivyo wengi wao wanazungumza lugha ya kihan, yaani Kichina. Watu wa Hui wanaoishi pamoja na watu wa makabila mengine madogo pia wanaweza kuzungumza lugha za makabila hayo. Baadhi ya watu wa Hui wanafahamu Kiarabu na Kiajemi. Tokea karne ya 7, wafanyabiashara wa kiarabu na kiajemi walikuja China, na kukaa katika miji ya Guangzhou, Quanzhou na mingine iliyoko pwani ya kusini mashariki mwa China, baada ya karne kadhaa, kikundi hicho cha watu hatua kwa hatua kimekuwa sehemu ya kabila la Hui. Mwanzoni mwa karne ya 13, watu wa Asia ya kati, waajemi na waarabu waliolazimishwa kuhamia sehemu ya kaskazini magharibi mwa China kutokana na vita nchini kwao waliishi pamoja na watu wa kabila la Han, Uigur na Mongolia kwa njia ya ndoa na dini, na kuunda kabila la Hui. Watu wa Hui ni waumini wa dini ya kiislamu, misikiti ilijengwa katika miji, vitongoji na vijiji vyote ambako wanaishi wahui. Watu wa Hui wana desturi maalum ya chakula na vinywaji, mikahawa na maduka ya chakula yanayowahudumia watu wa Hui yapo katika sehemu mbalimbali nchini kote. Watu wa Hui wana kiwango cha juu cha uchumi na utamaduni, na wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya historia ya China.

Kabila la Miao  

Kabila la Miao lina idadi ya watu milioni 8.94, wengi wao wanaishi katika mikoa ya Guizhou, Yunnan, Sichuan, Guangxi, Hunan, Hubei na Guangdong. Kabila la Miao linatumia Kimiao, ni lugha ya mfumo wa Han-Tibet. Zamani kabila la Miao halikuwa na herufi za maandiko za lugha yao. Mwaka 1956, lilifanya mageuzi kwa lahaja nne na tutunga herufi za lugha yao kwa hahaja ya kilatin. Miao ni moja ya makabila yenye historia ndefu nchini China, kuna maandishi kuhusu kabila hilo kwenye vitabu vya historia vilivyochapishwa miaka zaidi ya 4000 iliyopita. Kwa mujibu wa maandishi hayo, mfalme wa "Huang" na mfalme wa "Yan" walianzisha vita dhidi ya "Chi You" ambaye alikuwa mhenga wa watu wa Miao. Kutokana na vita, njaa, magonjwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu na kuachishwa kilimo mashamba yao, watu wa Miao walikuwa wakihamahama, na kusambaa katika sehemu nyingi kwa hivyo kuna tofauti kubwa kati ya vikundi mbalimbali vya watu wa Miao katika lahaja, mavazi, mapambo ya kichwani pamoja na mila na desturi. Watu wa Miao wanaoishi sehemu mbalimbali wanajiita kwa majina tofauti ya kikabila kutokana na umaalum wao wa mavazi kama vile "wamiao wa sketi ndefu", "wamiao wa sketi fupi", "wamiao wekundu" na "wamiao weusi". Watu wengi wa Miao ni wanaamini a dini ya kiasili ambayo kila kitu kina roho yake. Watu wa Miao wanalima mpunga na mahindi kwa wingi, pia wanalima mimea ya kiuchumi kama vile miti ya "tung-tree" na mboga wa "cole" na miti shamba ya aina mbalimbali.

Kabila la Yi

Kabila la Yi lina idadi ya watu zaidi ya milioni 7.7, ambao wengi wanaishi katika mikoa minne ya Yunnan, Sichuan, Guizhou na Guangxi kusini magharibi mwa China. Wanatumia lugha ya Kiyi, ni mfumo wa "Han-Tibet", wanaoishi pamoja na watu wa Han wanajua Kichina. Kabila la Yi ni kabila lenye idadi kubwa ya watu na historia ndefu, watu wake wanaenea katika sehemu nyingi. Zaidi ya miaka 2000 iliyopita, makundi ya kabila la Di, Qiang yalioishi katika sehemu ya kaskazini mwa China yalihamia kusini na kujiunga na wenyeji wa huko na kuunda kabila jipya la Yi. Kabila la Yi ulishikilia mfumo wa utumwa kwa kipindi kirefu. Baada ya kuasisiwa kwa China mpya mwaka 1949, mfumo wa utumwa katika jamii ya Yi ulitoweka hatua kwa hatua baada ya mageuzi ya kidemokrasia. Watu wa Yi waliamini miungu wengi, na dini ya Tao. Mwishoni mwa karne ya 19, dini ya kikristo ilienea hadi katika sehemu walikoishi, lakini wakristo ni wachache.



Kabila la Mongolia  

Kabila la Mongolia lina idadi ya watu zaidi ya milioni 5.8, wanaishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Mongolia ya ndani, na wilaya zinazojiendesha za kabila la Mongolia katika mikoa ya Xinjiang, Qinghai, Gansu, Heilongjiang, Jilin na Liaoning. Wanazungumza Kimongolia, ambacho ni mfumo wa lugha za Altai. Jina la "Mongolia" lilianzia katika enzi ya Tang, wakati ule, lilikuwa moja ya makundi mengi ya Mongolia ya sasa. Chanzo cha kundi hilo lilikuwa katika sehemu ya ukanda wa mashariki wa mto Erguna, baadaye lilihamia sehemu ya magharibi. Makundi mbalimbali ya Mongolia yalinyang’anyana watu, mifugo na mali, na kupigana vita bila kusita. Mwaka 1206, Tiemuzhen aliteuliwa kuwa kiongozi wa kundi la Mongolia, ambaye alipewa jina la mfalme "Chengjisihan". Tokea hapo, nchi ya Mongolia iliasisiwa na kabila la Mongolia lenye nguvu, utulivu na maendeleo likatokea rasmi katika sehemu ya kaskazini ya China.. Baadaye "Chengjisihan" aliunganisha makundi mbalimbali ya Mongolia, kuunganisha China na kuunda enzi ya Yuan. Watu wa Mongolia ni waumini wa dini ya Lama. Kabila la Mongolia limefanya mchango mkubwa katika sekta za siasa, jeshi, uchumi, sayansi na teknolojia, elimu ya falaki na hesabu, utamaduni , sanaa na matibabu.