Makabila Yenye Idadi ya Watu Wasiozidi Laki Moja

Radio China Kimataifa

China ina makabila 20 madogo yenye idadi ya watu wasiozidi laki moja, makabila hayo ni Bulang, Tajik, Achang, Pumi, Ewenk, Nu, Jing, Kinuo, Deang, Baoan, Russia, Yugu, Uzbek, Menba, Elunchun, Dulong, Tataer, Hezhe, Gaoshan na Luoba. 

Kabila la Luoba

Kabila la Luoba lina idadi ya watu takriban 3000, ni kabila lenye watu wachache kabisa nchini China. Wanaishi katika sehemu ya kusini mashariki ya mkoa unaojiendesha wa Tibet. Watu wa Luoba wanaoishi katika kaskazini ya wilaya ya Motuo wanazungumza Kitibet, wengine wanazungumza Kiluoba. Kiluoba ni lugha ya mfumo wa Hgan-Tibet, kuna tofauti kati ya lahaja za waluoba wanaoishi katika sehemu tofauti. Neno la Luoba linaasilia lugha ya Kitibet, maana yake ni "watu wa kusini". Kabla ya kuasisiwa kwa China mpya mwaka 1949, watu wa Luoba bado walirekodi mambo kwa kuchonga mbao au kufunga kamba, hawakuwa na maandishi, ni watu wachache tu waliojua Kitibet. Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, watu wa Luoba walipewa haki ya usawa na makabila mengine. Chini ya msaada wa serikali na makabila mengine, wameanzisha maisha mapya kwa njia ya kisiasa uzalishaji mali, na kupata maendeleo ya kiuchumi na kiutamaduni. Waluoba wengi ni waumini wa dini ya kiasili.



Kabila la Dulong 

Kabila la Dulong lina idadi ya watu zaidi ya 7400, wanaishi katika bonde la mto Dulong, wilaya inayojiendesha ya kabila la Dulong na kabila la Nu mkoani Yunnan. Wanazungumza Kidulong, lugha ya mfumo wa Han-Tibet, lakini haina herufi za maandishi. Wadulong wanaamini kuwa kila kitu kina roho, na kuabudu vitu vya kimaumbile. Mwanzoni kabila la Dulong liliitwa "Qiao". Katika enzi ya Ming na Qing liliitwa "Qiu" au "Qu". Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, lilianza kuitwa "Dulong" kutokana na matakwa yao wenywe. Zamani, watu wa Dulong walitumia vifaa duni vya kiasili katika uzalishaji wa kilimo, kukusanya matunda na kuvua samaki. Baada ya kuasisiwa kwa China mpya mwaka 1949, wadulong walibadili hali hiyo duni ya uzalishaji mali. Watu wa Dulong ni wachapa kazi, wakarimu na wenye moyo wa kirafiki , na wanapenda kuwasaidia wengine wenye dhiki. Katika shughuli za uwindaji, mawindo hugawanyika kwa washirika wote. Watu wa Dulong ni watu wenye uaminifu na kufuata ahadi na maadili.



Kabila la Kinuo

Kabila la Kinuo lina idadi ya watu zaidi ya elfu 20, wanaishi kwenye mlima mrefu ulioko katika wilaya ya Xishuangbanna ya mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China. Wanazungumza Kikinuo, ambacho ni lugha ya mfumo wa Han-Tibet, lugha hiyo haina herufi za maandishi. Watu wa Kinuo zamani waliamini kuwa, kila kitu kina roho, na kuabudu wahenga. Hakuna maandishi kuhusu chanzo cha kabila la Kinuo. Watu wa Kinuo wanamwabudu Zhu Geliang, inasemekana kuwa, walikuwa sehemu ya askari wa jeshi la Zhu Geliang, walihamia kutoka kaskazini wakati lilipopiga vita kusini. Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, wakinuo waliingia katika jamii ya ujamaa moja kwa moja kutoka jamii ya asili, na kubadili kabisa hali duni ya uzalishaji wa kilimo, kurekodi mambo kwa kuchonga kwenye mianzi, kufanya biashara ya kiasili ya kubadilishana vitu kwa vitu na kutibu magonjwa kwa kutoa sadaka. Hivi sasa kabila la Kinuo limekuwa na makada, madaktari, wafanyabiashara na wafundi wa kilimo.



 


Kabila la Elunchun

Kabila la Elunchun lina idadi ya watu zaidi ya 8000, wanaishi katika sehemu ya milima ya Xinanling mpakani mwa mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani na mkoa wa Heilongjiang. Katika tarafa ya Hulunber ya mkoa wa Mongolia imeanzishwa wilaya inayojiendesha ya kabila la Elunchun. Watu wa Elunchun wanazungumza Kielunchun, ni lugha ya mfumo wa Altai, ambayo haina herufi za maandiko, wote wanatumia lugha ya kihan, yaani Kichina. Maana ya "Elunchun" ni watu wanaoishi mlimani. Watu wa Elunchun zamani waliishi maisha kwa kuwinda wanyama, kuchuma matunda na kuvua samaki. Karibu wanaume wote ni wapanda farasi na wapiga mshale hodari, wanafahamu sana desturi na utaratibu wa maisha wa wanyama wa aina mbalimbali, wana uzoefu mwingi wa uwindaji. Hadi miaka ya 40 ya karne ya 20, walikuwa bado ni kabila la kuhamahama na kuwinda, mawindo hugawanyika kwa wastani, hata wazee, wadhaifu, na walemavu. Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, watu wa Elunchun waliingia katika jamii ya ujamaa moja kwa moja. Hivi sasa wameacha maisha ya kuhamahama na uwindaji, na kujenga makazi, wakiwa kama walinzi wa misitu na wanyamapori. Watu wa Elunchun ni watu wenye akili na busara, wanaweza kutengeneza sanaa za mikono zenye nakshi nyororo kwa kutumia maganda ya miti ya Birch, kama vile nguo, viatu, sanduku, vikapu, mapipa, hata mashua nyepesi. Watu wa Elunchun ni waumini wa dini ya Shaman, wanaabudu wahenga na vitu vya kimaumbile,wanaamini kuwa kila kitu kina roho.



Kabila la Tataer

Kabila la Tataer lina watu karibu 5000, wanaoishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Uigur wa Xinjiang, wengi wanaishi katika miji ya Yining, Tacheng na Urumqi. Wana lugha yao ya Kitataer, ni lugha ya mfumo wa Altai. Licha ya wazee, watataer wengi huzungumza lugha ya Kikhazak au Kiuigur. Kabila la Tataer lina maandiko ya herufi za kiarabu, lakini kutokana na kuishi pamoja na watu wa Khazak na Uigur, pia wanatumia maandiko ya makabila hayo mawili. Wa-tataer wengi ni waumini wa dini ya kiislamu. Mapema wakati wa enzi ya Tang, wa-tataer walitokana na kabila la "Dadan" kutoka nchi ya Turki iliyoko kaskazini mwa China. Katika karne ya 13, watu wa Mongolia walipofanya vita vya kuvamia sehemu ya magharibi, watu wa Ulaya waliwaita wamongolia "Tataer". Kuanzia mwanzoni mwa karne ya 19, baadhi ya wa-tataer walihamia mkoani Xinjiang kutoka Russia. Baada ya vita kuu ya pili ya dunia, wa-tataer wengine waliendelea kuhamia mkoani Xinjiang na kuanzisha rasmi kabila la Tataer la China. Wa-tataer wanaishi vijijini hushughulikia ufugaji na wa-tataer wasomi hasa walimu wanaishi mijini na kutoa mchango mkubwa kwa elimu ya mkoa wa Xinjiang.