Sera ya Kikabila ya China

Radio China Kimataifa

China ni nchi ya muungano yenye makabila mengi. Serikali ya China inatekeleza sera ya usawa, umoja na kusaidiana, kuheshimu na kulinda imani ya dini ya makabila madogo pamoja na mila na desturi zao.

Mfumo wa kujiendesha katika maeneo ya makabila madogo ni moja ya mifumo muhimu ya kisiasa nchini China. Hii inamaanisha kuwa, chini ya uongozi wa serikali kuu, inaweza kuanzisha mikoa au wilaya zinazojiendesha katika maeneo ya makabila madogo, kuweka ofisi za madaraka na kutekeleza madaraka ya kujiendesha katika mikoa au wilaya hizo. Serikali kuu inahakikisha kutekeleza sheria na sera za kitaifa kutokana na hali halisi ya kienyeji katika maeneo ya makabila madogo; kuwaandaa makada wengi, na wafundi wa aina mbalimbali; wakazi wa makabila mbalimbali wanaoishi katika sehemu zinazojiendesha kama wachina wengine wanajishughulisha na ujenzi wa kisasa wa kijamaa wa China, kuharakisha maendeleo ya uchumi wa kienyeji, na kukuza utamaduni na kujenga sehemu zinazojiendesha zenye umoja na usitawi wakiwa chini ya uongozi wa chama cha kikomunisti cha China.

Kutokana na uzoefu wa miongo kadhaa iliyopita, yaani chama cha kikomunisti cha China kikiwa kama chama tawala kimetunga sera mbalimbali kuhusu suala la kikabila kama zifuatazo:

Uundaji, ukuaji na utowekaji wa makabila ni mwendo mrefu wa kihistoria, suala la kikabila litakuwepo kwa kipindi kirefu.

Awamu ya ujamaa ni kipindi cha kustawi kwa pamoja kwa makabila mbalimbali, vipengele vya pamoja vya makabila mablimbali vimeongezeka, lakini umaalum na tofauti kati ya makabila bado yapo.

Suala la makabila ni sehemu moja ya masuala yote ya kijamii, na litatatuliwa hatua kwa hatua katika mwendo wa kutatua masuala yote ya kijamii, hivyo suala la kikabila la China la hivi sasa litatatuliwa hatua kwa hatua katika juhudi za pamoja za kujenga ujamaa.

Bila kujali idadi ya watu, historia ndefu au fupi na kiwango cha maendeleo, makabila yote yametoa mchango katika ustaarabu wa China, hivyo yanapaswa kupata haki ya usawa. Tunapaswa kuimarisha umoja wa makabila mbalimbali na kulinda muungano wa taifa.

Kuleta ongezeko la uchumi ni jukumu la kimsingi la awamu ya ujamaa, pia ni jukumu la kimsingi la kazi ya kikabila la China katika kipindi cha hivi sasa. Makabila mbalimbali yanatakiwa kusaidiana ili kuleta maendeleo na usitawi wa pamoja.

Kuanzisha sehemu zinazojiendesha katika eneo la makabila ni mchango mkubwa uliotolewa na Chama cha Kikomunisti cha China kwa nadharia ya kikabila ya Maxism, ni utaratibu wa kimsingi wa kutatua suala la kikabila nchini China.

Jambo muhimu linalotakiwa kufanywa katika kushughulikia vizuri mambo ya kikabila na kutatua suala la kikabila ni kuwaandaa makada wengi wa makabila madogo wenye akili na maadili.

Suala la makabila hufungamana na suala la kidini, hivyo inapaswa kutekeleza sera ya dini ya taifa kwa pande zote na kwa njia sahihi wakati wa kushughulikia masuala yote ya makabila.

Aidha, serikali ya China inaposhughulikia kuhimiza maendeleo ya eneo la makabila madogo katika sekta za uchumi, utamaduni na elimu, na kuinua hali ya maisha na utamaduni ya watu wa makabila madogo , inapaswa kuheshimu imani zao za dini, na kuhifadhi urithi wao wa kiutamaduni. Imefanya sensa, kukusanya data, kufanya utafiti na kuchapisha vitabu kuhusu urithi wa kiutamaduni na urithi wa kidini na sanaa za kienyeji za makabila mbalimbali. China imetenga fedha nyingi katika kukarabati mahekalu na majengo ya kidini yenye thamani ya kihistorai na kiutamaduni katika eneo la makabila madogo.