Uchumi wa Kikabila Nchini China

Radio China Kimataifa

Kutokana na kuongezeka kwa uchumi nchini China, uchumi wa eneo la makabila madogo pia umepata maendeleo makubwa.

Ufugaji unachukua sehemu kubwa katika uchumi wa eneo la makabila madogo. Kuanzia miaka ya 80 ya karne ya 20, China imetekeleza sera ya kusaini mkataba wa kutunza mifugo na malisho kwa wafugaji, na kuimarisha ujenzi wa mbuga na mfumo wa usimamizi. Hivi sasa, katika sehemu za malisho za mikoa ya Qinghai, Gansu, Sichuan, Xinjiang, Ningxia na Mongolia, uzalishaji wa mifugo umepata maendeleo makubwa. Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa China imezalisha mifugo milioni 100 katika sehemu za malisho na sehemu za nusu kilimo na nusu ufugaji. Na katika baadhi ya sehemu, kumekuwa na malisho ya familia. Kutokana na uendeshaji na uzalishaji mifugo kwa kiwango kikubwa na kutumia njia ya sayansi na teknolojia, uzalishaji wa mifugo na ufanisi wa malisho ya kifamilia umeinuka kwa kiwango kikubwa.

Miji ya eneo la makabila madogo ina rasilmali na shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi, ni vituo muhimu vya kukuza uchumi wa makabila madogo. Kuanzia miaka ya 80 ya karne 20, uchumi wa miji katika eneo la makabila madogo pia umepata maendeleo makubwa. Takwimu zinasema kuwa, hivi sasa katika sehemu zinazojiendesha za makabila madogo kuna viwanda au makampuni milioni moja na kuanzisha kimsingi mfumo wa viwanda, ambao viwanda vya kisasa, viwanda vya watu binafsi, biashara na utoaji huduma zinakuwepo sambamba. Kiwango cha miji katika mikoa ya Mongolia, Qinghai, Ningxia na Xinjiang kimezidi kile cha wastani cha miji mingine nchini China, miji hiyo imetoa mchango mkubwa katika kuongoza uchumi wa sehemu za makabila madogo.

Uchumi usio wa serikali pia umefanya kazi kubwa katika kukuza uchumi wa miji katika sehemu za makabila madogo. Kwa mfano, mwishoni mwa karne iliyopita, uchumi usio wa serikali wa mkoa wa Qinghai ulichukua asilimia 40 ya pato la mkoa huo.

Zaidi ya hayo, katika mchakato wa kufungua mlango kwa nchi za nje, miji kadhaa ya eneo la makabila madogo imezidisha maingiliano na ushirikiano wa kiteknolojia kati yao na nchi za nje. Hivi sasa katika sehemu za makabila madogo yamechomoka makampuni makubwa yanayojulikana nchini hata duniani, yakiwemo kampuni ya kutengeneza nguo za sufi ya Eerduosi ya mkoa unaojiendesha wa kabila la Mognolia ya ndani, na kampuni ya Tianye ya mkoa unaojiendesha wa kabila la Uigur.