Sayansi na Teknolojia ya Makabila Madogo ya China

Radio China Kimataifa

Ili kuhimiza maendeleo ya sayansi na teknolojia katika sehemu za makabila madogo, serikali ya China imechukua sera mbalimbali maalum, kama vile kuwaandaa mafundi wa kazi mbalimbali, kuandikisha wanafunzi wa makabila madogo au kuandaa darasa la kikabila katika vyuo vikuu. Baadhi ya vyuo vikuu vimeanzisha kozi mpya kutokana na mahitaji ya makabila madogo, ili kuharakisha kazi ya kuwaandaa mafundi wa aina mbalimbali wa makabila madogo. Na hali kadhalika kuingiza wataalamu na zana za kisasa, ili kurekebisha uzalishaji wa viwanda vya jadi na bidhaa za jadi, na kuleta ufanisi wa kiuchumi, kuanzisha mfumo wa kueneza sayansi na teknolojia katika sehemu za malisho vijijini; kutunga sera ya kuwahimiza watu wenye ujuzi kufanya kazi katika sehemu za makabila madogo. Sehemu zilizoendelea kuongeza msaada kwa sehemu za makabila madogo. Hivi sasa mashirika mengi ya utafiti wa kisayansi yameanzishwa katika sehemu za makabila madogo, na kuunda mfumo kamili wa kufanya utafiti wa kisayansi na kuwaandaa wasomi wenye taaluma.

Takwimu zinasema kuwa, hivi sasa China imekuwa na wanasayansi na wahandisi laki moja kutoka sehemu za makabila madogo. Wafanyakazi wa sayansi na teknolojia wa makabila madogo wamekuwa nguvu muhimu za kuhimiza maendeleo ya sayansi na teknolojia ya China, kati yao wako wataalamu wa Taasisi ya Sayansi ya China na Taasisi ya Uhandisi ya China, na waliotoa mchango mkubwa katika kuhimiza matumizi ya sayansi na teknolojia. Kwa mfano mtaalamu wa kabila la Hui wa Taasisi ya Sayansi bwana Wang Shiwen kwa miaka mingi anashughulikia utafiti, matibabu na ufundishaji kuhusu ugonjwa wa moyo na matibabu ya dharura, amefanya mchango mkubwa katika kuenedeleza matibabu ya wazee nchini China. Mtaalamu wa kabila la Zhuang wa Taasisi ya Uhandisi ya China Bi. Wei Yu aliyepata shahada ya udaktari katika chuo kikuu cha Aachen cha Ujerumani, amekuwa mmoja wa wavumbuzi katika eneo jipya la viumbe wa elektroniki na hesabu ya viumbe. Mtaalamu wa kilimo wa kabila la Korea Zheng Huiyu, amefanya utafiti kuhusu upandaji wa kunde soya kwa miaka mingi na kufaulu kuotesha mbegu bora maarufu.