Elimu ya Makabila Madogo ya China

Radio China Kimataifa

Elimu ni msingi wa maendeleo ya sayansi na teknolojia. Serikali ya China imechukua hatua na sera maalum kukuza elimu ya kikabila, kama vile, kufuatilia na kusaidia kukuza elimu ya makabila madogo, kuanzisha idara maalum ya kusimamia elimu ya makabila madogo, kuheshimu haki za makabila madogo na sehemu zinazojiendesha za makabila madogo kujiamulia kukuza elimu ya kikabila; kufuatilia ufundishaji wa lugha ya kikabila na ya lugha mbili, kuiamrisha ujenzi wa vitabu vya kiada vya lugha ya kikabila; kufanya juhudi kuwaandaa walimu wa makabila madogo; kutoa kipaumbele kwa makabila madogo katika kutenga fedha; kuendesha vyuo vikuu vya kikabila vya aina nyingi, kuwapa utunzi maalum wanafunzi wa makabilka madogo na kuzishirikisha sehemu zilizoendelea kusaidia sehemu za makabila madogo.

Serikali ya China imechukua hatua mbalimbali kukuza elimu ya shile katika sehemu ya makabila madogo, kujenga shule za msingi, sekondari, na vyuo vikuu, na kuzingatia umaalum wa kikabila, kutumia lugha ya kikabila katika shule za msingi na sekondari za sehemu za makabila madogo yenye lugha na herufi za maandiko yake. Idadi ya wanafunzi wa makabila madogo imeonegezeka kwa kiasi kikubwa katika shule za aina mbalimbaliu nchini China. Aidha, kuna vyuo vikuu vya kikabila katika sehemu ya kaskazini maghairbi, kaskazini mashariki na kusini magharibi zenye makabila mengi madogo, vyuo vikuu hivyo vimewaandaa wanafunzi wengi kutoka makabila madogo.

Takwimu zinaonesha kuwa, hivi sasa makabila 55 madogo nchini China yote yana wanafunzi wao wenye shahada kwanza, shahada ya pili, na ya udaktari.