Utamaduni wa Kikabila wa China

Radio China Kimataifa

Ili kurithi na kutukuza utamaduni wa makabila madogo, sehemu mbalimbali zinazojiendesha za makabila madogo kutokana na hali halisi yao zimeanzisha mashirika ya waandishi, opera, muziki, dansi, uchoraji, filamu na upiga picha. Baadhi ya vyuo vya makabila madogo pia vimeanzisha kozi ya fasihi ya kikabila, sehemu nyingine zimeanzisha shule za sanaa, kama vile chuo cha muziki, chuo cha uigizaji mchezo, na chuo cha filamu, na kuwaandaa watu wengi wanaoshughulikia shughuli za fasihi na sanaa. Na mikoa ya Tibet, Xinjiang na Mongolia imeanzisha vyuo vya matibabu ya kikabila.

Hivi sasa, China imekuwa na kundi la waandishi na wasanii wa makabila madogo, wakiwemo mwandishi wa kabila la Man Lao She, mtungaji shairi wa kabila la Dai Kan Langying na mwandishi wa kabila la Hezhe Wu Baixin. Vikundi mbalimbali vya maonyesho ya sanaa vya makabila madogo vimeundwa, wachezaji wao wanashughulika katika vijiji, malisho na miji ya makabila madogo.

Vitabu vingi kuhusu fasihi na sanaa za kienyeji za makabila madogo vimechapishwa, kama vile “Mkusanyiko wa nyimbo za kienyeji za China”, “Mkusanyiko wa opera na muziki wa China”, “mkusanyiko wa ala za muziki za kienyeji za makabila madogo wa China”, “Mkusanyiko wa dansi za kienyeji za makabila madogo nchini China”, “mkusanyiko wa hadithi za kienyeji nch8ini China”, “mkusanyiko wa methali nchini China” na kadhalika.

Uchapishaji wa majarida ya fasihi na sanaa za makabila madogo pia umepata maendeleo. Hivi sasa China imekuwa na majaribu makubwa zaidi ya 100 kuhusu fasihi na sanaa za makabila madogo mbalimbali, kati ya majaribu hayo, majaribu zaidi ya 20 yanachapishwa kwa maandishi ya lugha za makabila madogo. Vitabu, magazeti na majaribu yaliyochapishwa na sehemu zinazojiendesha za makabila vimeongezeka kwa kiwango kikubwa, na vitabu 3400 vilichapishwa kwa lugha ya makabila madogo.