Hali ya Dini Nchini China

Radio China Kimataifa

China ni nchi yenye dini mbalimbali. Waumini wa dini wa China niwa dini za kibudha, kidao, kiislamu, na kikristo.

Kutokana na takwimu zisizokamilika, hivi sasa China ina waumini zaidi ya milioni 100 wa dini za aina mbalimbali, makanisa, misikiti na mahekalu zaidi ya elfu 85, wafanyakazi wa shughuli za kidini laki tatu, vikundi zaidi ya 3000 na vyuo 74 vya kidini.

Nchini China, kuna Shirikisho la Dini ya kibudha la China, Shirikisho la Dini ya Kidao la China, Shirikisho la Dini ya Kiislamu la China, Shirikisho la Dini ya Uzalendo la Kikatoliki la China, Jumuiya ya Maaskofu wa Katoliki ya China, Kamati ya Harakati za Uzalendo ya Dini ya Kikristo ya China na Shirikisho la Ukristo ya China. Mashirika mbalimbali ya kidini yanachagua viongozi na kuunda miundo ya utawala kutokana katiba zao yenyewe; yanashughulikia mambo yao ya kidini kwa kujiendesha, kuanzisha vyuo vya kidini kutokana na mahitaji yao, kuchapisha vitabu vya kidini na majarida ya kidini na kuanzisha shughuli za kuhudumia jamii.