Mawasiliano ya Kidini na Nje

Radio China Kimataifa

Dini za kibudha, kiislamu na kikristo zote zilienea nchini China kutoka ng’ambo, zote ni za kimataifa, zina hadhi muhimu duniani, na zina waumini wengi katika nchi na sehemu nyingi duniani, baadhi yao hata zimetangazwa kuwa dini ya kitaifa katika nchi kadhaa.

Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, mawasiliano na nje katika mambo ya kidini yanaendelezwa kwa haraka. Kwa mfano, waumini wa dini ya kibudha wa China mara kwa mara wanafanya shughuli za mawasiliano ya dini za kienyeji na waumini wa dini ya kibudha wa Thailand, Korea ya Kusini, Japan, Mnyamnar, Sri lanka na Vietnam. Katika miaka ya karibuni, sarira ya Budha wa China yaliwahi kuabudiwa nchini Thailand, Mnyamnar, Sri Lanka na nchi nyingine, waumini wa dini ya kibudha wa Thailand na wa mkoa wa Tibet wa China wameanzisha mfumo wa kufanya maingiliano kuhusu taaluma za elimu ya dini ya kibudha kila baada ya muda fulani.

Zaidi ya hayo, ujumbe wa mashirikiano ya kidini ya China unazitembelea mara nyingi nchi za Ulaya magharibi na Amerika Kaskazini kutokana na mwaliko, si kama tu wajumbe wamejifahamisha mambo ya dini ya nchi hizo, bali pia kuwafahamisha watu wa huko mambo ya dini ya China.