中国国际广播电台
Majengo ya jadi ya Kichina ni
sehemu muhimu ya utamaduni mkubwa
unaong’ara wa China, aina za
majengo hayo pamoja na ya Kimagharibi
na ya Kiarabu ni aina tatu muhimu
za majengo duniani.
Majengo ya jadi ya Kichina
ni majengo pekee yanayojengwa
kwa mbao, na yanaonesha fikra
za watu wa China kuhusu maadili
ya jamii na mtazamo wa uzuri.
Kutokana na utamaduni wa jadi,
aina za majengo ya Kichina
zimegawanyika kama ifuatayo:
majengo yanayotukuza mamlaka
ya kifalme, majengo hayo yanaonekana
zaidi katika ujenzi wa makasri
na mpango wa ujenzi wa mji
mkuu; mkazo unatiliwa zaidi
kwenye uzuri wa jumla wa seti
ya majengo, na kuyafanya majengo
kwenye pande mbili za mstari
wa katikati yalingane, na
kulingana na mazingira ya
kimaumbile.
Mbali na majengo ya kabila
la Wahan, kuna aina nyingi
za majengo ya makabila madogo
madogo ambayo zinachangia
uzuri wa mfumo wa ujenzi wa
Kichina.
Majengo hayo yamegawanyika
katika aina tano, nazo ni
majengo ya kasri, majengo
ya mahekalu, majengo ya bustani
na majengo ya makaburi.
Katika historia ya China,
sanaa na ufundi wa majengo
ya Kichina iliwahi kuathiri
ujenzi wa majengo ya Kijapan,
Kikorea, Kiviet Nam na Kimongolia.
Leo majengo ya Kichina licha
ya kuendelea na mtindo wake
wa jadi pia yameingiza sanaa
za majengo ya Kimagharibi
na kuziendeleza.
|