中国国际广播电台
Majengo ya bustani nchini
China yana historia ndefu,
na ni majengo maarufu duniani.
Mapema miaka 3000 iliyopita
kulikuwa na bustani ya kifalme
nchini China. Tokea hapo bustani
zilianza kuwepo katika miji
mikuu ya enzi mbalimbali na
miji mingine mikubwa. Kuna
aina nyingi za bustani nchini
China ambazo ni muhimu katika
mifumo mitatu mikuu ya ujenzi
wa bustani duniani.
Bustani nchini China huwa
na milima na maji kwa ajili
ya kuleta uzuri wa kimaumbile.
Majengo ya bustani nchini
China yanagawanyika katika
fungu la bustani za kifalme
na bustani binafsi. Bustani
hizo zilijengwa kwa milima
ya bandia na maziwa, maua
na miti, nyua za nyumba, na
ujia wenye paa na mbao zenye
maandishi, bustani yenye mzingira
hayo ni kama bustani ya peponi.
Bustani nchini China zimegawanyika
kwa dhana za aina tatu, yaani
dhana za utawala wa kifalme,
dhana za mandhari ya kichimbakazi
(fairyland) na dhana za mandhari
ya kufananisha na hali ya
maumbile.
Mandhari ya kichimbakazi
yanazingatia kuleta mazingira
ya utawa, mazingira ambayo
yalifuatwa sana na waumini
wa dini ya Dao ya Kichina.
Mazingira kama hayo pia yanaonekana
katika ujenzi wa mahekalu
na bustani za kifalme.
Mandhari ya kufananisha na
maumbile yanajengwa kwa kufuata
hisia za wenye bustani. Mandhari
za namna hiyo zinapatikana
zaidi katika bustani za wasomi.
Tofauti kubwa kati ya bustani
za Kichina na za Kimagharibi
ni kuwa bustani za Kimagharibi
zinajengwa kwa kuonesha uzuri
wa majengo, na bustani za
Kichina zinajengwa kwa nia
ya kuonesha uzuri wa mandhari
ya kimaumbile na hisia za
wenye bustani.
Bustani katika Mji wa
Suzhou
Bustani kadhaa mjini Suzhou
ziliorodheshwa katika kumbukumbu
ya urithi wa dunia mwaka 1997.
Bustani katika mji huo zimeingiza
sifa zote za bustani nchini
China. Bustani hizo zimekuwa
na miaka zaidi ya 2000, na zilizobaki
sasa ziko 10. Bustani katika
mji wa Suzhou nyingi ni ndogo,
lakini kutokana na kuwa ndani
yake kuna milima ya bandia na
maziwa, miti na maua, madaraja
madogo na vibanda, bustani hizo
zinaonekana mandhari kubwa ya
kimaumbile na kufanya watu wahisi
wako kwenye mazingira ya utamaduni
mkubwa.
Bustani
ya Kifalme Yuanmingyuan
Bustani hiyo ya kifalme ilikuwa
na mchanganyiko wa mitindo
ya Kichina na Kimagharibi.
Hii ilikuwa ni bustani nzuri
kuliko zote nchini China.
Lakini mwaka 1860 bustani
hiyo iliteketezwa na muungano
wa wavamizi wa Uingereza na
Ufaransa. Hivi sasa watu wanaweza
tu kukisia jinsi ilivyokuwa
nzuri kwa kuangali magofu
yake.
Bustani ya Kifalme ya Yuanmingyuan
iko katika kitongoji cha Beijing
upande wa kaskazini magharibi.
Bustani hiyo licha ya kuwa
bustani nzuri kuliko bustani
nyingine za kifalme pia imewahi
kujulikana hata barani Ulaya
kutokana na maelezo ya barua
za wamisionari na ilikuwa
na athari kwa ujenzi wa bustani
za Ulaya.
|