中国国际广播电台
Majengo husifiwa kama ni “muziki
uliotulia”, ni aina moja ya
utamaduni wa binadamu. Majengo
ya kale nchini China mengi ni
ya mbao ya kabila la Wahan na
pia kuna majengo mengine mazuri
ya makabila madogo madogo. Mtindo
wa majengo ya Kichina ulipevuka
nchini China kutoka karne ya
pili mpaka karne ya 19, usanii
wake umejaa utamaduni mkubwa.
Sanaa za ujenzi wa Kichina ni
moja ya sanaa zenye historia
ndefu, ambayo ipo katika sehemu
nyingi nchini China. Na sanaa
hiyo iliathari ujenzi wa majengo
hata nchini Japan, Korea na
Viet-Nam, na baada ya karne
ya 17 iliwahi kuathiri hata
ujenzi wa majengo ya Ulaya.
China ni nchi kubwa yenye makabila
mengi, wahenga wa China walijenga
majengo yenye miundo na mitindo
tofauti kutokana na mazingira
na jiografia tofauti. Kwenye
mabonde ya mto Huanghe, kaskaizni
mwa China, wahenga walijenga
nyumba kwa mbao na udongo ili
kukinga upepo wa baridi na theluji;
lakini katika sehemu ya kusini
ya China, kutokana na joto wahenga
walijenga nyumba kwa mianzi
na matete, na ili kukwepa unyevunyevu,
nyumba husimamishwa kwa nguzo
na kuacha chini wazi; kwenye
sehemu za milima, wahenga walikuwa
wakijenga nyumba kwa mawe.
Ujenzi wa kale nchini China
uliwahi kupamba moto katika
vipindi vitatu, navyo ni enzi
za Qin na Han, enzi za Sui na
Tang na enzi za Ming na Qing.
Katika vipindi hivi vitatu,
majengo mengi mazuri yalitokea
yakiwa ni pamoja na kumbi za
kifalme, makaburi, majengo ya
kukinga maadui na majengo ya
uhandisi wa kuhifadhi maji.
Kati ya majengo hayo ukuta mkuu
uliojengwa na Qinshihuang (mfalme
wa kwanza wa Enzi ya Qin), daraja
la Zhaozhou lililojengwa katika
Enzi ya Sui (581-618), na kasri
la kifalme lililojengwa katika
enzi za Ming na Qing mjini Beijing,
mpaka sasa majengo hayo yanavutia
sana kutokana na hekima za watu
wa kale wa China.
Lakini
kwa sababu ya miaka mingi,
uharibifu wa mvua na upepo,
vita, baadhi ya majengo ya
kale yametoweka, na yaliyobaki
sasa yaliyo mengi ni ya baada
ya Enzi ya Tang (baada ya
karne ya 7). Yafuatayo ni
maelezo kuhusu majengo hayo.
|