中国国际广播电台
Enzi ya Tang (618-907) ni kipindi
ambacho uchumi na utamaduni
katika jamii ya kimwinyi nchini
China ulifikia kwenye kilele,
ufundi na sanaa za ujenzi wa
majengo pia zilikuwa zimeendelea
sana. Majengo katika Enzi ya
Tang yalikuwa makubwa na ya
adhama.
Majengo katika Enzi ya Tang
yalikuwa ni makubwa, na mpangilio
wa fungu la majengo ni wa
busara. Katika mji mkuu wa
Enzi ya Tang, Chang An (mji
wa Xi’an kwa leo), na mji
wa Luoyang kuna makasri makubwa
na majumba ya maofisa. Mji
wa Chang An ulikuwa mji mkubwa
duniani katika enzi hiyo,
na mpangilio wa majengo yake
ulikuwa wa busara kabisa katika
miji yote ya China ya kale,
ndani ya mji huo kasri la
Daming lilikuwa na eneo zaidi
ya mara tatu kuliko Kasri
la Kifalme la Beijing.
Majengo katika Enzi ya Tang
yanaonesha sayansi ya muundo
wa mbao, mshikamano baina
ya nguzo na maboriti umeonesha
ushirikiano mzuri wa nguvu.
Ukumbi wa Buddha katika Hekalu
la Foguang mlimani Wutaishan
umeonesha wazi mtindo wa majengo
ya Enzi ya Tang.
Kadhalika, majengo ya matofali
na mawe pia yalikuwa yameendelea
sana katika Enzi ya Tang,
mifano ya majango hayo ni
pagoda ya Dayanta, pagoda
ya Xiaoyanta na pagoda ya
Qianxunta katika mji wa Xi’an.
|