中国国际广播电台
Enzi ya Yuan (1206-1368) nchini
China ilikuwa ni dola la kifalme
lililoundwa na watawala wa kabila
la Wamongolia, lakini katika
enzi hiyo, majengo hayakuwa
na maendeleo, na majengo mengi
yalikuwa ya kawaida kutokana
na kuzorota kwa uchumi na utamaduni.
Mji mkuu wa Enzi ya Yuan,
Dadu (sehemu ya kaskazini
ya Beijing kwa leo) ni mwanzo
wa mji mkuu wa enzi mbili
za Ming na Qing, Beijing.
Shughuli za ujenzi katika
mji mkuu huo zilikuwa hasa
katika ujenzi wa majengo ya
ukumbi na bustani, Bustani
ya Beihai ya leo mjini Beijing
ni kumbukumbu halisi ya enzi
hiyo.
Katika Enzi ya Yuan dini
ilikithiri sana, hasa dini
ya Buddha ya madhehebu ya
Kitibet, kwa hiyo mahekalu
ya dini yalikuwa mengi.
Majengo ya mbao katika Enzi
ya Yuan yaliurithi ufundi
wa enzi iliyotangulia ya Song,
lakini kutokana na uchumi
uliokuwa mbaya na uhaba wa
magogo, majengo katika enzi
hiyo yalikuwa ya kawaida yakilinganishwa
na majengo ya Enzi ya Song
iwe kwa ukubwa au kwa umakini.
|