Enzi ya Qing (1616-1911) ni
enzi ya mwisho ya kifalme nchini
China. Majengo katika enzi hiyo
mengi zaidi yalirithi mtindo
wa enzi iliyotangulia ya Ming
ingawa yalitokea mabadiliko
kidogo ya kufanya majengo yawe
ya kifahari zaidi.
Mji wa Beijing katika enzi hiyo
ulikuwa sawa na enzi ya Ming.
Kwenye kuta za mji kuna malango
20 na ndani ya mji kuna makasri
makubwa. Katika enzi hiyo bustani
nyingi za kifalme zilijengwa,
kati ya bustani hizo zilizo
kubwa na maarufu ni bustani
ya Yuan Ming Yuan na kasri la
majira ya joto (Summer Palace).