Muhtasari wa Majengo ya Kisasa
中国国际广播电台

      
Majengo ya kisasa yanamaanisha majengo yaliyojengwa kuanzia katikati ya karne ya 19 hadi sasa.

Tokea vita vya kasumba vya mwaka 1840 hadi Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, majengo yenye mtindo wa Kichina na wa Kimagharibi yalitokea nchini China. Katika kipindi hiki majengo ya mtindo wa Kichina yanaendelea kuwa mengi, lakini nyumba za michezo, mahoteli, maduka, na maduka makubwa yalikuwa hujengwa kwa mchanganyiko wa mitindo ya Kichina na ya Kimagharibi na majengo ya aina ya Kimagharibi yalitokea katika miji ya Shanghai, Tianjin, Qingdao na Harbin kwenye sehemu zilizokodiwa na nchi za nje, na pia majengo ya ubalozi, benki za nchi za nje na mahoteli na klabu za nchi za nje zilitokea katika miji hiyo.

Baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, ujenzi umeingia katika kipindi kipya cha kihistoria, kutokana na jinsi uchumi ulivyoendelea kwa haraka ujenzi wa majengo uliongezeka. Katika kipindi hiki majengo makubwa 10 yenye mapaa ya aina ya kasri la kifalme yalijengwa katika mwaka wa maadhimisho ya miaka kumi tokea Jamhuri ya Watu wa China iasisiwe. Tokea miaka ya 80 ya karne iliyopita, majengo yameanza kuwa na aina kwa aina.