中国国际广播电台
Liang Sicheng
Liang
Sicheng (1901—1972), mwaka 1915
hadi 1923 alisoma katika Chuo
Kikuu cha Qinghua mjini Beijing,
mwaka 1927 alipata shahada ya
pili na mwaka 1948 alipata shahada
ya daktari katika chuo kikuu
kimoja cha Marekani. Maishani
mwake alitoa mchango mkubwa
katika elimu na majengo.
Liang Sicheng alianza kutafiti
majengo ya kale ya China katika
miaka ya 30 ya karne iliyopita
na aliandika makala nyingi
zenye thamani kubwa kuhusu
utaalamu wa majengo ya kale
ya China.
Liang Sicheng alitoa mashauri
mengi kuhusu mpangilio wa
majengo ya mji wa Beijing,
aliwahi kushiriki kazi ya
kusanifu nembo ya taifa na
mnara wa mashujaa wa China
katika uwanja wa Tian An Men.
Liang Sicheng alikuwa mmoja
wa watangulizi waliofanya
utafiti wa majengo ya kale
ya China, makala zake za utafiti
zina thamani kubwa katika
nyanja ya ujenzi.
Wu Liangyong
Wu Liangyong alizaliwa mwaka
1922, aliwahi kuwa mwenyekiti
wa Shirikisho la Kimataifa la
Ujenzi (UIA) na mwenyekiti wa
Shirika la Makazi ya Dunia (WSE).
Aliwahi kutoa mashauri mengi
kuhusu majengo ya Kichina na
mpangilio ya majengo ya miji.
Usanifu wake wa nyumba zenye
ua wa mraba katika kichochoro
cha Ju Er mjini Beijing ulipata
tuzo ya Shirika la Makazi ya
Binadamu la Umoja wa Mataifa
mwaka 1992, na mwaka 1993 alitoa
sayasi ya mazingira ya makazi
ya binadamu, na mwaka 1996 alipata
tuzo ya Shirikisho la Wasanifu
Majengo la Kimataifa.
Zhang Kaiji
Zhang
Kaiji ni msanifu majengo wa
awamu ya kwanza baada ya Jamhuri
ya Watu wa China kuasisiwa.
Alizaliwa mwaka 1912 mjini Shanghai,
na mwaka 1935 alihitimu katika
Chuo Kikuu cha Nanjing, aliwahi
kuwa msanifu mkuu majengo katika
taasisi ya usanifu majengo ya
Beijing na naibu mkurugenzi
wa bodi ya Shirikisho la Wasanifu
Majengo la China, na mwaka 1990
alipata sifa ya “Msanifu mkuu
wa Majengo”, mwaka 2000 alipata
“tuzo ya Majengo ya Liang Sicheng”.
Aliwahi kusanifu jukwaa la kuangalia
gwaride katika uwanja wa Tian
An Men, jumba la makubusho ya
mapinduzi ya China na jumba
la makubusho ya historia ya
China, jumba la wageni wa kitaifa
na jumba la unajimu la Beijing.
Yang Tingbao
Yang Tingbao (1901—1982),
alihitimu katika Chuo Kikuu
cha Qinghua mjini Beijing,
na alibakizwa kuwa mwalimu
katika chuo chake na wakati
huo alitumwa na chuo chake
kwenda Marekani kuendeleza
zaidi masomo. Alipokuwa Marekani
alipata tuzo ya kwanza katika
mashindano ya usanifu ya Emerson
(Emerson Prize Competition)
mwaka 1924, na mwaka huo pia
alipata tuzo ya kwanza ya
mashindano ya Shirikisho la
Sanaa ya Manispaa (Municipal
Art Society Prize Competition).
Tokea mwishoni mwa miaka
ya 20 ya karne iliyopita,
aliwahi kusanifu benki ya
mawasiliano ya Beijing, hospitali
kuu ya Nanjing, maktaba ya
Chuo Kikuu cha Qinghua, Chuo
Kikuu cha Shenyang, Hoteli
ya Amani ya Beijing, na pia
aliwahi kushiriki katika usanifu
wa ukumbi mkuu wa umma mjini
Beijing, kituo cha garimoshi
cha Beijing, maktaba ya Beijing
na ukumbi wa kumbukumbu ya
Mwenyekiti Mao mjini Beijing.
Majengo yake yalitiliwa mkazo
muunganisho wa mitindo ya
Kichina na ya kimagharibi.
|