Chuo Kikuu cha Tsinghua
Radio China Kimataifa


Chuo Kikuu cha Tsinghua mjini Beijing ni chuo kikuu cha kitaifa maarufu kabisa cha utafii na elimu za mseto kinachojulikana kwa kozi za sayansi na uhandisi, kina historia ya miaka mia moja hivi, ni moja ya vituo muhimu vinavyowaandaa wasomi wenye kiwango cha juu nchini China.

Hivi sasa, Chuo Kikuu cha Tsinghua kina vitivo 44 katika taasisi 11 za sayansi, ujenzi, uhandisi wa hifadhi maji, uhandisi wa mitambo, sayansi na teknolojia ya upashanaji habari, utamaduni na sayansi ya jamii, usimamizi wa uchumi, sheria, uchoraji picha, usimamizi wa mambo ya umma na kadhalika. Kozi zake za ujenzi, kompyuta, magari, fizikia na nyinginezo zinajulikana sana nchini China. Katika miaka 20 iliyopita, Chuo Kikuu cha Tsinghua kinajiendeleza kuwa chuo kikuu cha mseto wa elimu, kimeongeza kozi za usimamizi, Kichina na uandishi wa habari, na kiko mbioni kuanzisha chuo cha utibabu.

Hivi sasa Chuo Kikuu cha Tsinghua kina wahadhiri na maprofesa 7100, wanafunzi zaidi ya elfu 20, ambapo wanafunzi elfu kumi kati yao wa shahada ya pili na ya utakdari. Wanafunzi wengi wa wanafunzi wa ng’ambo wanapenda kusoma katika chuo kiuu hicho.

Chuo Kikuu cha Tsinghua kinajulikana nchini na duniani kutokana na kiwango cha juu cha utaalamu na ubora wa elimu. Kama ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Tsinghua, soma tovuti: http://www.tsinghua.edu.cn