Chuo Kikuu cha Fudan
Radio China Kimataifa


Chuo Kikuu cha Fudan kiko mjini Shanghai, mji mkubwa kabisa wa viwanda na biashara nchini China, ni moja ya vyuo vikuu maarufu vya mseto wa elimu nchini China, pia ni moja ya vyuo vikuu vyenye historia ndefu nchini China.

Hivi sasa chuo kikuu hicho kina kozi nyingi ambazo ni pamoja na utamaduni, sayansi za jamii na maumbile, teknolojia, usimamizi na utibabu. Kina vitivo 72 katika taasisi 15 ambavyo ni pamoja na chuo cha uandishi wa habari, chuo cha sayansi ya maisha, chuo cha utibabu cha Shanghai na chuo cha software. Pia kina taasisi 65 za utafiti, na vituo 91 vya utafiti unaoshughulikia zaidi ya kozi moja. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Fudan kimekuwa moja ya vituo vyenye sifa nzuri ya kitaaluma duniani, kimeanzisha ushirikiano na maingiliano na vyuo vikuu na taasisi za utafiti zaidi ya 200 kutoka nchi na sehemu 30 hivi.

Chuo Kikuu cha Fudan sasa kina wanafunzi elfu 25, na wanafunzi 1650 wa nchi za nje. Kama ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu chuo kikuu hicho, soma tovuti yake:http://www.fudan.edu.cn/