Chuo Kikuu cha Zhongshan
Radio China Kimataifa


Chuo Kikuu cha Zhongshan kiko katika mji wa Guangzhou, mji mkuu wa mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, ni chuo kikuu mchanganyiko wa elimu. Chuo kikuu hicho kilianzishwa mwaka 1924 na Bwana Sun Yat-sen , kiongozi maarufu wa mapinduzi ya demokrasia ya China.

Chuo Kikuu cha Zhongshan kina kozi 79 katika taasisi 19 ambazo ni pamoja na taasisi ya utamaduni, taasisi ya Lingnan, taasisi ya hisabati na sayansi ya kompyuta na taasisi ya utibabu. Chuo kikuu hicho kina maabara na kituo cha utafiti chenye zana za kisasa. Chuo kikuu hicho kina wanafunzi elfu 41 wa elimu aina mbalimbali, kati ya hao kuna wanafunzi elfu 17 wa shahada ya kwanza, wanafunzi 5440 wa shahada ya pili, wanafunzi 1970 wa shahada ya udaktari, na wengine 450 kutoka nchi za nje. Sehemu mpya ya Chuo cha Lingnan cha Chuo Kikuu cha Zhongshan ina mandhari nzuri na zana za kisasa, inasifiwa kuwa ni moja ya sehemu zinazopendeza zaidi katika vyuo vikuu nchini China. Maktaba ya Chuo Kikuu cha Zhongshan ni moja ya maktaba zenye vitabu vingi katika sehemu ya kusini mashariki China. Ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Zhongshan, soma tovuti yake:http://www.zsu.edu.cn/