Chuo Kikuu cha Wuhan
Radio China Kimataifa


Chuo Kikuu cha Wuhan kiko mjini Wuhan, mji mkuu wa mkoa wa Hubei katikati ya China. Hiki ni moja ya vyuo vikuu vya mseto wa elimu na utafiti chenye kozi nyingi. Chuo Kikuu cha Wuhan kina kozi 105 katika vitivo 11 vya falsafa, uchumi, sheria, elimu, fasihi, historia, sayansi, uhandisi, kilimo, utibabu na usimamizi. Chuo kikuu hicho kina walimu zaidi ya 5000 na waanfunzi zaidi ya elfu 45, miongoni mwao kuna wanafunzi elfu 12 wa shahada ya pili na ya udaktari. Katika miaka ya hivi karibuni, Chuo Kikuu cha Wuhan kimewaalika wasomi na wanasiasa maarufu 300 wa nchini na ng’ambo kuwa maprofesa wake wa heshima, na kuanzisha ushirikiano na maingiliano na vyuo vikuu na taasisi zaidi ya 200 za utafiti wa kisayansi za nchi na sehemu zaidi ya 60.

Chuo Kikuu cha Wuhan iko kwenye mteremko wa mlima wa Luojia, inasifiwa kuwa ni moja ya chuo kikuu cha kupendekeza zaidi nchini China. Ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Wuhan, soma tovuti ya mtandao: http://www.whu.edu.cn/