Chuo Kikuu cha Zhejiang
Radio China Kimataifa


Chuo Kikuu cha Zhejiang kiko mjini Hanzhou, mji mkuu wa mkoa wa Zhejiang, kusini mashariki mwa China. Hiki ni moja ya vyuo vikuu vya utafiti vyenye kiwango kikubwa na kozi nyingi zaidi nchini China, na kinajulikana duniani.

Kozi za Chuo Kikuu cha Zhejiang ni pamoja na falsafa, uchumi, sheria, elimu, fasihi, historia, sayansi na uhandisi, kilimo, matibabu na usimamizi. Kuna kozi 108 za shahada ya kwanza. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Zhejiang kina walimu zaidi ya 8700 na wanafunzi zaidi ya elfu 40, kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 9700 wanasomea shahada ya pili, wanafunzi 4200 wanasomea shahada ya udaktari na wanafunzi zaidi ya 1000 kati ya hao wanatoka nchi za nje.

Chuo Kikuu cha Zhejiang kimepata mafanikio makubwa ya taaluma katika kozi za uchumi, sheria na sayansi. Eneo la jumla la maktaba yake linafikia mita za mraba elfu 59, ina vitabu milioni 5.91, ni moja ya maktaba kubwa ya vyuo vikuu vyenye mchanganyiko wa elimu nchini China. Ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Zhejiang, soma tovuti yake:http://www.zju.edu.cn/